DKT. TAX APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO ZA MABALOZI WA ZAMBIA, BRAZIL NA VATICAN
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amepokea nakala za Hati za Utambulisho za mabalozi wateule wa nchi za Zambia, Brazil na Vatican. Mhe. Waziri Tax amepokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Zambia nchini, Mhe. Mathew Jere, Balozi mteule wa Brazil nchini, Mhe. Gustavo Martins Nogueira na Balozi Mteule wa Vatican Nchini, Mhe. Askofu Mkuu Angelo Accattino leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Akizungumza na mabalozi hao kwa nyakati tofauti Waziri Tax amewahakikishia ushirikiano kutoka Serikalini wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao ya kibalozi hapa nchini. Pia Waziri Tax ametoa rai kwa mabalozi hao kuendeleza na kudumisha ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na nchi zao. “Tanzania na Zambia tumekuwa marafiki na ndugu wa muda mrefu, Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na Serikali ya Zambia katika sekta za biashara na uwekezaji kwa maslahi mapana ya pande zote mbili,” alisema Dkt. Tax B