JNHPP KUONDOA CHANGAMOTO ZA UPUNGUFU WA UMEME- EWURA
Na Mwandishi Wetu Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) linalojengwa Rufiji mkoani Pwani litaondoa changamoto za upungufu wa umeme nchini na mradi huo unategemewa kuzalisha megawati 2115 pindi utakapokamilika Juni 2024. Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya siku moja katika mradi huu, Mwenyekiti wa Bodi hiyo Profesa Mark Mwandosya amesema, mradi wa JNHPP ni wa kisasa kwa sababu ni mradi mkubwa ukilinganisha na miradi mingine ambayo imeshajengwa lakini pia utazalisha umeme kwa kiwango kikubwa na utawezesha watanzania kupata umeme wa uhakika. “Kama nilivyosema uzalishaji wa umeme utakuwa mkubwa kwa hiyo kwa miaka mingi sitegemei kwamba tutakuwa na uhaba wa upatikanaji wa umeme. Umeme ni mfumo lakini pia mambo mengine yanayoambatana na nayo ni njia za kusambaza umeme, njia za kupeleka umeme kwenye vyanzo. "Sasa lazima kila wakati kuwe