Posts

WAZIRI MKUU ATAKA UMAKINI MANUNUZI YA VIFAA VYA UJENZI WA MIRADI

Image
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka Halmashauri nchini kuongeza umakini katika manunuzi ya vifaa vinavyotumika katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao ili iweze kukamilika katika muda uliopangwa na kutoa huduma kwa wananchi. Ametoa wito huo leo (Jumanne, Novemba 29, 2022) alipozungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Kisarawe, Mkoani Pwani. Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Wenyeviti wa Halmashauri wanapaswa kuwa wakali katika  kufuatilia manunuzi ya vifaa mbalimbali na watumie wakaguzi wa ndani katika kufuatilia taarifa za manunuzi. “Manunuzi hapa kisarawe ni ya gharama kubwa katika miradi yenu, miradi haishi kwasababu ya gharama kubwa, na bahati mbaya mnafanya hivyo kwa fedha za Serikali kuu” Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ameiagiza Taasisi ya Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kumfuatilia aliyekuwa afisa mapato katika Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Fredy Bandai aliyehamishiwa Mtwara vijijini “Huyu asimamishwe kazi na arejeshwe Kisarawe ili aje atolee taarifa

MAJALIWA: UWEKEZAJI NCHINI HAUTAKWAMA

Image
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kuwaunga mkono wawekezaji ili kuhakikisha uwekezaji wao haukwami bali unakua na kuleta tija. Amesema hayo jana (Novemba 28, 2022) alipotembelea na kuweka jiwe la msingi la kiwanda cha  kutengeneza mabati cha Lodhia kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani. Mheshimiwa Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha wawekezaji nchini wanapata faida “tunathamini uwekezaji huu, tunaheshimu uwekezaji huu na tutakuunga mkono kwenye uwekezaji. Amesema kuwa Wawekezaji wamekuwa na mchango mkubwa katika kuchangia marndeleo ya nchi katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya, elimu, kilimo, mawasiliano na hata ajira “ Upanuzi wa kiwanda hiki ni kumuunga mkono Rais Samia katika jitihada zake za kuendelea kupunguza changamoto ya upatikanaji wa ajira kwa watanzania” Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa uwepo wa wawekezaji ikiwemo katika sekta ya viwanda wanaisaidia nchi kwa kiasi

WANANCHI KIBITI WAMSHUKURU RAIS SAMIA UJENZI DARAJA LA MBUCHI

Image
Wakazi wa Kata za Mbuchi na Mbwera Kibiti Mkoani Pwani wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa daraja la Mbuchi linalounganisha kata hizo ambalo limegharimu shilingi bilioni 7.2. Wamezungumza hayo leo (Jumatatu, Novemba 28, 2022) wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea kukagua ujenzi wa daraja hilo lenye urefu wa mita 61. Wakizumgumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema kuwa ujenzi wa daraja hilo umesaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa adha ya usafiri kati ya kata hizo ambapo awali iliwalazimu kutumia mitubwi ambayo ilikuwa tishio kwa uhai wa wakazi hao hasa kipindi cha mvua kubwa mto huo ukiwa imejaa. “Sisi kina mama tuliteseka kwa muda mrefu sana, safari za kwenda kufuata huduma za afya kwetu ilikuwa ni mtihani mkubwa, tulihofia maisha yetu, lakini kwasasa hata usiku wa manane tunavuka bila shida kufuata huduma za afya, tunamshukuru sana Rais wetu kwa kuiona changamoto yetu na kuifanyia kazi” Akizungumza na wanamchi baada ya k

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMANNE NOVEMBA 29, 2022

Image
 

RAIS MWINYI AHUTUBIA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA UTALII HUKO RIYADH, SAUDI ARABIA

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akihutubia kongamano la Kimataifa kuhusu utalii jijini Riyadh, Saudi Arabia leo Novemba 28, 2022. Rais Mwinyi amehutubia kongamano hilo la 22 la World Travel & Tourism Council Global Summit, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Taarifa kamili iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasilisho ya Rais Ikulu ya Zanzibar na kusainiwa na Mkurugenzi wake Charles Hilary inafafanua zaidi hapo chini.  

RAIS WA ZANZIBAR DKT HUSSEIN MWINYI KUHUTUBIA KONGAMANO LA KIMATAIFA KUHUSU UTALII

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuhutubia katika Kongamano la Kimataifa la 22 la World Travel & Tourism Council Global Summit linalofanyika katika Hoteli ya Ritz-Carlton Riyadh, Saudi Arabia.  Katika Kongamano hilo la Kimataifa Rais Dk. Mwinyi anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.