Posts

RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA MSALATO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na Wananchi kabla ya kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, Mkoani Dodoma tarehe 30 Oktoba, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa pamoja na Meneja Mkaazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa upande wa Tanzania Dkt. Patricia Leverley kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi Mradi wa Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, Mkoani Dodoma tarehe 30 Oktoba, 2022. Wengine katika picha ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson pamoja na viongozi wengine wa Chama na Serikali.  

MTANZANIA ASHINDA TAJI LA UREMBI KWA VIZIWI DUNIANI

Image
Mrembo wa Tanzania Hadija Kanyama ametwaa taji la urembo la dunia kwa viziwi katika shindano lililofanyika Dar es Salaam na kutangazwa ushindi huo na jopo la majaji 8 wakiongozwa na Rais wa Mashindano hayo kutoka nchini Marekani, Mama Baneta Ann Li.  

TUKAANZISHE KLINIKI ZA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA- DKT. KENGIA.

Image
 Na WAF- DOM.  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa jamii na lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. James Kengia ametoa wito kwa wataalamu wa afya  kwenda kuanzisha kliniki za magonjwa yasiyoambukiza katika vituo vyao vya kutolea huduma. Dkt. Kengia amesema hayo wakati akifunga mafunzo ya magonjwa yasiyoambukiza yaliyoratibiwa na Wizara ya Afya, OR TAMISEMI pamoja na Wadau wa chama cha Kisukari Tanzania (TDA) kwa Watoa huduma (Madaktari, Wauguzi) pamoja na wakufunzi Jijini Dodoma.  Amesema, ni matarajio kwamba elimu iliyotolewa kwa siku tano itaenda kuwekwa kwa vitendo ili kuleta mabadiliko katika kutatua changamoto za magonjwa yasioambukiza nchini, ikiwemo namna ya kutambua na kuwahudumia wagonjwa wa magonjwa yasiyoambukiza. Ok "Tutakaporudi vituoni tuhakikishe tunaanzisha kliniki za magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa vituo ambavyo havina na kublresha kliniki hizo kwa maeneo ambayo zipo tayari, kazi hii ifanywe kwa ushirikiano na wauguzi ambao pia nimepata taarif

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAPILI OKTOBA 30, 2022

Image
 

RAIS SAMIA AKUTANA NA RAIS WA TOTAL ENERGIES KATIKA MASUALA YA UTAFITI NA UZALISHAJI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katikka pucha na Rais wa Kampuni ya TotalEnergies katika masuala ya Utafiti na Uzalishaji Nicolas Terraz mara baada ya mazungumzo yao, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 29 Oktoba, 2022 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipeana mikono na Rais wa Kampuni ya TotalEnergies katika masuala ya Utafiti na Uzalishaji Nicolas Terraz mara baada ya mazungumzo yao, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 29 Oktoba, 2022 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Kampuni ya TotalEnergies katika masuala ya Utafiti na Uzalishaji Nicolas Terraz mara baada ya kuwasili pamoja na ujumbe wake Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 29 Oktoba, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais wa Kampuni ya TotalEnergies katika masuala ya Utafiti na Uzalishaji Nicolas Terraz mara baada ya mazungumzo yao, Ikulu Chamwino Mkoani Dodom

CP SUZANE KAGANDA AAPISHWA

Image
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura, tarehe 28.10.2022 amemuapisha Kamishna wa Utawala na Rasilimali Watu CP Suzane Salome Kaganda baada ya kupandishwa cheo na kuteuliwa kuwa Kamishna wa Utawala na Rasilimali Watu. IGP Wambura amemuapisha kwa niaba ya Mhe. Rais na Amiri Jeshi Mkuu na hafla ya uapisho imefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi, Makao Makuu ya Polisi Dodoma

MAENEO YALIYOMEGWA KWENYE HIFADHI YAPANGIWE MPANGO WA MATUMIZI YA ARDHI

Image
  Na  Munir Shemweta, WANMM NJOMBE Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ametaka maeneo ya yanayomegwa kwa ajili ya kupatiwa wananchi waliovamia hifadhi yapangiwe mpango wa matumizi ya ardhi na kutolewa hati kwa wamiliki wake. Dkt mabula alitoa kauli hiyo oktoba 27, 2022 katika kijiji cha Mpanga kilichopo wilaya ya Wanging'ombe wakati timu ya mawaziri nane wa wizara za kisekta inayoshughulikia migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 ilipotembelea mkoa wa Njombe ikiwa ni  mfululizo wa ziara zake kawenye mikoa ya Tanzania Bara. Kijiji cha Mpanga ni moja ya vijiji 11 vilivyopo wilaya ya Wanging'ombe na Makete mkoani Njombe ambavyo vimemegewa eneo kutoka hifadhi ya Pori la Akiba la Mpanga Kipengele. Dkt Mabula alisema, serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeridhia baadhi ya vijiji kwenye mkoa wa Njombe kubaki maeneo ya hifadhi za Mapori ya Akiba ingawa wananchi wake waliingia bila ridhaa ya serikali. Kwa mujibu wa Dkt Mabu

SERIKALI KUIMARISHA USHIRIKIANO NA WADAU KATIKA USIMAMIZI WA MAAFA

Image
  SERIKALI   KUIMARISHA   USHIRIKIA N O  N A   WADAU   KATIKA   USIMAMIZI   WA   MAAFA N A.MWADISHI   WETU Serikali   kupitia   Ofisi   ya   Waziri   Mkuu   Idara   ya  Menejimeti ya  Maafa   imeeleza   itae n delea   kuimarisha   ushirikia n o  n a wadau   wa   masuala   ya   maafa  n chi ni  ili   kue n delea  kusimamia na  kuratibu masuala   ya   maafa nchini ili   kuedelea   kupunguza madhara yatokanano na maafa.   Akiwasilisha hotuba kwa niaba ya mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa wakati wa mkutano wa wadau wa masuala ya Afya Moja uliofanyika katika Ukumbi wa Edema Mkoani Morogoro  B i.Valentina Sanga alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha masuala ya maafa yanaratibiwa na kusimamiwa kwa ufanisi kwa kushirikiana   na wadau m b alim b ali.   Mkuta n o huo ulihusisha wawakilishi kutoka katika wizara mbalimbali za kisekta , Ofisi ya Makamu wa Rais,   Ofisi ya  Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ,  Wizara  ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Afya, Wizara ya Kilimo, wawakili