Posts

WAZIRI MKUU MAJALIWA NA MKEWE MARY WASHIRIKI KATIKA MAZISHI YA KITAIFA YA WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA JAPAN SHINZO ABE JIJINI TOKYO

Image
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary leo Septemba 27, 2022 wameshiriki katika mazishi ya kitaifa ya aliyekuwa Waziri Mkuu Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo  Abe yaliyofanyika Tokyo nchini Japan. Wengine walioshiriki katika mazishi hayo ni mke wa Balozi wa Tanzania nchini Japan, Consolata Luvanda, Balozi wa Tanzania nchini Japan, Baraka Luvanda na kulia ni Naibu Waziri wa  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk.

MWENYEKITI WA CCM, NA RAIS WA TANZANIA, NDUGU SAMIA AONGOZA KIKAO CHA NE

Image
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Samia Suluhu Hassan, ameongoza Kikao Maalum cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), kilichoketi katika ukumbi wa NEC (White House), leo Septemba 27, 2022 Makao Makuu ya CCM Dodoma.    

WAKAZI WAJITOKEZA KWA WINGI ZIOEZI LA UTATUZI WA MIGOGORO YA ARDHI LIKIENDELEA JIJINI DODOMA

Image
  Na Anthony Ishengoma-Dodoma.   Wakazi takribani 150 wa Kata ya Mkonze Jijini Dodoma wamejitokeza mbele  ya Kamati  iliyoundwa na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Allan Kijazi iliyo jikita Jijini Dodoma kuhakikisha inamaliza kero zote za ardhi ndani ya Jiji la Dodoma. Wakazi hao wamejitokeza kwa makundi tofauti kutoka mitaa ya kata ya Mkonze ambapo zoezi limeanzia ili  kuwasilisha malalamiko yao mbele ya kamati hiyo uku madai yao yakitofautiana kulingana na aina ya migogoro ambayo kila mwananchi anakabiliana nayo. Akifafanua kuhusu aina ya malalamiko ambayo Kamati imeyabaini baada ya kukutana na Wananchi wa  Kata hiyo Kamishna wa Ardhi wa Ardhi Nchini Nathaniel Methew alisema mpaka sasa Kamati imebaini  kuwa kuna  migogoro muda mrefu ambayo ilianza tangu enzi za Mamlaka ya Ustawishaji  Makao Makuu Dodoma CDA hivyo kutoa taswira tofauti ya namna migogoro hiyo uilivyojitokeza. Kamishna Methew aliongeza kuwa pia timu yake imebaini pia migogoro hiyo u

TANZANIA NA UAE ZATIA SAINI MKATABA WA KUTOTOZA KODI MARA MBILIKUBALI KATI YA NCHI HIZO

Image
  Na Benny Mwaipaja, Dubai SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa   Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu zimetia saini   mkataba   wa makubaliano ya kuondoa utozaji Kodi Mara Mbili na Kuzuia Ukwepaji wa Kodi ya Mapato kati ya nchi hizo mbili, yaani Agreement on Avoidance of Double Taxation and Prevention of Fiscal Evasion on Income Taxes. Mkataba huo umetiwa saini katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Umoja wa Falme za Kiarabu mjini Dubai na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Mhe. Mohamed Bin Hadi Al Hussain, Waziri wa Nchi wa Mambo ya Fedha wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alisema kuwa kusainiwa kwa Mkataba huo ni jitihada za Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alizozifanya Mwezi Februari, 2022 katika nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu ambapo aliagiza kuondolewa kwa changamoto hiyo ili kukuza mahusiano ya kiuchumi, kuimarisha

IGP WAMBURA NA WAKUU WENZAKE WALA VIAPO TUME YA UTUMISHI WA YA MAJESHI YALIYO CHINI YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Image
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Camilius Wambura akila kiapo cha kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi, Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Mheshimiwa Gerson Mdemu, jijini Dodoma leo Septemba 26, 2022. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini, CGP Mzee Ramadhani Nyamka akila kiapo cha kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi, Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Mheshimiwa Gerson Mdemu, jijini Dodoma leo Septemba 26, 2022. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamad Khamis Hamad akila kiapo cha kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi, Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Mheshimiwa Gerson Mdemu, jijini Dodoma leo Septemba 26, 2022. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Miriam Mmbaga aki

ZIARA YA MAKAMPUNI YA KIMAREKANI KUJIONEA FURSA ZA UWEKEZAJI TANZANIA YAANZA

Image
    NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM   BALOZI wa Marekani nchini Mhe. Dkt. Donald J. Wright na Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe, wamezindua rasmi ziara ya makampuni ya Kimarekani kutembelea Tanzania Bara na Zanzibar kujionea fursa za kibiashara na uwekezaji (Business Fact-Finding Mission). Makampuni 20 ya Kimarekani yalijisajili kushiriki katika ziara hii inayolenga kuangazia biashara za kilimo, nishati, huduma za afya na viwanda vya teknolojia ya habari na mawasiliano. Katika hafla ya uzinduzi wa ziara hiyo, Balozi Wright aliyapongeza makampuni hayo kwa uamuzi wao wa kuiangalia Tanzania kama mahali wanapoweza kuwekeza katika sekta muhimu za uchumi na kupanua biashara zao.   “Tunakaribisha ushiriki zaidi wa Wamarekani katika uchumi wa Tanzania – kwa hakika, hili ni mojawapo ya malengo ya msingi kabisa ya ubalozi wetu.   Makampuni ya Kimarekani huja na ubunifu, ujuzi na mtaji lakini pia nia ya kuwafundisha Watanzania jinsi ya kusimamia na kuendesha bi

JAPAN KUNUNUA KILO MILIONI 30 ZA TUMBAKU TANZANIA

Image
  KAMPUNI ya Japan Tobacco Incorporation (JTI) imeahidi kununua kilo milioni 30 za tumbaku kutoka kwa wakulima wa Tanzania katika msimu ujao wa kilimo.   Ahadi hiyo imetolewa leo (Jumatatu, Septemba 26, 2022) na Rais na Mtendaji Mkuu wa JTI, Bw. Masamichi Terabatake mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyetembelea ofisi zao ili kuwahakikishia utekelezaji wa mazungumzo yaliyofanyika wakati wa mkutano wa TICAD 8, jijini Tunis, Agosti, mwaka huu.   Akizungumza baada ya kikao hicho, Waziri Mkuu amesema uamuzi wa kampuni hiyo kuongeza kiwango cha ununuzi wa tumbaku utatoa ahueni kwa wakulima wa Tanzania ambao walikuwa hawana uhakika wa soko la zao hilo.   “Leo Bodi ya Wakurugenzi imetangaza uamuzi wa kununua kilo milioni 30 za tumbaku kutoka kilo milioni 14 ambazo walinunua msimu uliopita. Hii ni fursa kubwa kwa wakulima wetu kwani kiasi hicho ni zaidi ya uzalishaji wa zao la tumbaku Tanzania,” amesema.   “Miaka ya nyuma makampuni yaliyokuwa yakinunua tumbaku yalizoea kuwapangia wakulima

MWENYEKITI WA CCM RAIS SAMIA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU MAALUM YA CCM, IKULU CHAMWINO JIJINI DODOM

Image
  MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan alipowasili katika ukumbi wa Chamwino Dodoma kwa ajili ya kuongoza Kikao Maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika leo 26-9-2022. Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akihudhuria kikao cha Kamati Kuu cha kupitisha maombi ya wanachama wanaomba nafasi za uongozi wa Chama ngazi za wilaya , kinachofanyika Chamwino, Dodoma .  Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akihudhuria kikao cha Kamati Kuu cha kupitisha maombi ya wanachama wanaomba nafasi za uongozi wa Chama ngazi za wilaya , kinachofanyika Chamwino, Dodoma . Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM ambae ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao cha Kamati Kuu Maalum

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMANNE SEPTEMBA 27, 2022

Image