Posts

BORESHENI MAZINGIRA YA KAZI KIAFYA – KATAMBI

Image
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi ameuagiza uongozi wa Kiwanda cha Mbeya Cement kuhakikisha unatafuta mitambo ya  kisasa kwa ajili ya kudhibiti vumbi la saruji inayozalishwa kiwandani hapo. Mhe. Naibu Waziri Katambi ametoa agizo hilo Agosti 26, 2022 alipofanya ziara ya kushtukiza ya kukagua kiwanda hicho na kufuatilia utekelezaji wa sheria za kazi na masuala ya Usalama na Afya mahala pa kazi. ''Sijaridhishwa na hali niliyoikuta kimsingi eneo la uzalisha kuna vumbi ambalo limeshindwa kudhibitiwa na hivyo watumishi kuwa katika hatari kubwa ya kuugua magonjwa" Mhe. Katambi alisisitiza kuwa  usalama wa watu kazini ni muhimu na serikali itaendelea kusimamia sheria  ili Watanzania wafanye kazi katika hali ya usalama sehemu za kazi. ”Katika kipindi cha mwezi mmoja nahitaji kuona mabadiliko ya namna ya kudhibiti vumbi  ikiwa ni pamoja na  kuwepo kwa vifaa vya kujikinga na vumbi (barakoa)." Kwa upande wake, Mkuru

WAZIRI MKUU AHUDHURIA MKUTANO WA TICAD, TUNIS TUNISI

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa akifuatilia Mkutano wa Nane wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kimataifa kuhusu Maendeleo ya Japan na Afrika (TICAD 8) unaoendelea katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Palais des Congres mjini Tunis,Tunisia, Agosti 27, 2022. Waziri Mkuu anamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano huo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa akisalimiana na Rais wa Tunisia Kais Saied alipowasili katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Palais des Congres kuhudhuria Mkutano wa Nane wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kimataifa kuhusu Maendeleo ya Japan na Afrika (TICAD 8), mjini Tunis,Tunisia, Agosti 27, 2022. Waziri Mkuu anamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Tunisia, Mhe. Kais Saied alipowasili katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Palais des Congres kuhudhuria Mkutano wa Nane wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kimataifa kuhusu Maend

RAIS WA ZANZIBAR DKT HUSSEIN MWINYI APOKEA RIPOTI YA UKAGUZI HESABU ZA SERIKALI YA

Image
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2020/2021 na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.Dkt.Othman Abass Ali, hafla hiyo iliyofanyika leo 27-8-2022, katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.  

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAPILI AGOSTI 28, 2022

Image
 

SIMBA QUEENS YAWEKA HISTORIA, YATINGA FAINALI ZA CAF CHAMPIONS LEAGUE KWA SOKA LA WANAWAKE

Image
Simba Queens SC imefuzu kwenda Morocco kucheza fainali za CAF Champions League kwa soka la wanawake baada ya kuifunga She Corporate ya Uganda kwa goli 1-0 katika mchezo wa fainali wa Michuano ya mchujo ya CAF ukanda wa CECAFA, (CECAFA Zone Qualifiers) uliopigwa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi usiku wa kuamkia leo Agosti 28, 2022. Bao la Simba Queens SC lililofungwa na Vivian Corazone kwa mkwaju wa penati dakika ya 49, baada ya Asha Djafari kufanyiwa madhambi kwenye eneo la hatari. Michuano hiyo ya CAF Champions League Unatakiwa kuanza mwezi ujao, na  huwa inachezwa katika taifa moja ikijumuisha jumla ya timu 8, sita mabingwa kutoka zone sita za soka, nafasi moja ya Bingwa mtetezi na nyingine Bingwa wa nchi mwenyeji. Ukiacha ushindi huo Simba Queens SC pia pia imetoa Mchezaji Bora wa mashindano, Vivian Aquino Corazone na Golikipa Bora wa mashindano, Gelwa Yona. VivianCorazone Aquino, Mchezaji Bora wa Mashindano. Gelwa Yona, Kipa Bora wa Mashindano

NAIBU SPIKA ZUNGU AFUNGUA MAFUNZO YA UWAZI NA UWAJIBIKAJI KWA KAMATI ZA USIMAMIZI ZA BUNGE (PAC, LAAC NA PIC) PAMOJA NA KAMATI YA BAJETI.

Image
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa WAJIBU Institute of Public Accountability, Ndg. Ludovick Utouh kabla ya kufungua mafunzo ya uwazi na uwajibikaji kwa kamati za usimamizi za Bunge (PAC, LAAC na PIC) pamoja na kamati ya Bajeti yaliyofanyika leo tarehe 27 Agosti, 2022 katika hoteli ya Royal Village Jijini Dodoma. Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu akifungua mafunzo ya uwazi na uwajibikaji kwa kamati za usimamizi za Bunge (PAC, LAAC na PIC) pamoja na kamati ya Bajeti yaliyofanyika leo tarehe 27 Agosti, 2022 katika hoteli ya Royal Village Jijini Dodoma. Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa kamati ya Bajeti baada ya kufungua mafunzo ya uwazi na uwajibikaji kwa kamati za usimamizi za Bunge (PAC, LAAC na PIC) pamoja na kamati ya Bajeti yaliyofanyika leo tarehe 27 Agosti, 2022 katika hoteli ya Royal Village Jijini Dodoma Baadhi ya Wajumbe wa kamati za usimamizi wa