Posts

HALMASHAURI ZATAKIWA KUTENGA PESA ZA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WAVIU

Image
  NAIBU Ofisi yaWaziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga amepongeza Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa kupunguza kiwango cha maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka 3.5% mwaka 2020 hadi kufikia 3.2% kwa mwaka 2021. “Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye bajeti Mpya ya serikali 2022-2023 itakayoanza mwezi wa saba ameongeza fedha eneo kutoka Billion 1 Mpaka Billion 1.8” Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi yaWaziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga alipokuwa akipokea taarifa ya Mkoa wa Tanga ya Mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi. Aidha Naibu Waziri Mhe. Ummy Nderiananga ameshauri Halmashauri za wilaya kuona umuhimu wa kutenga fedha za Mapambano Dhidi ya Virusi vya Ukimwi. Hii itasaidia kuwawezesha katika miradi ya vikundi vya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi (WAVIU) kufanya shughuli zao za maendeleo vizuri. Wananchi msiogobe kujitokeza kupima virusi vya ukimwi, mpime mjitambue afya zenu. Kama Kauli mbiu inavyosema pima V

MITAMBO YA KMTC IKO SALAMA NA INAFANYA KAZI-DKT. KIJAJI

Image
 Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amesema mitambo iliyopo katika Kiwanda cha Kilimanjaro Machine tools (KMTC) iko salama na inaendelea kufanya kazi ya uzalishaji wa vipuri na mashine mbalimbali wakati maboresho ya kuendesha mitambo hiyo kielektroniki yanaendelea.  Waziri Kijaji ameyasema hayo alipofanya ziara katika Kiwanda cha KMTC kichopo Moshi Mkoani Kilimanjaro Mei 29, 2022 kujionea jinsi kiwanda hicho kinavyofanya kazi na mikakati iliyopo ya kukifufua ili kifanye kazi kwa ufanisi na kuzalisha bidhaa zinazokidhi mahitaji ya soko kwa kutumia teknolojia ya kisasa.  Akiwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah  pamoja na wajumne wengine aliziagiza Taasisi za TEMDO na CAMARTEC  kufanya kazi kwa kushirikiana na kiwanda hicho ili kiweze kuzalisha bidhaa kwa wingi zilizosanifiwa na Taasisi hizo.  Aidha, Waziri Kijaji alisema uboreshaji wa Kiwanda hicho ni muhimu kwa kuwa bidhaa za chuma zinahitajika katika m

KATIBU MKUU CCM AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO SHINYANGA, AHIMIZA UTUNZWAJI WA MIUNDOMBINU

Image
  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameendelea na ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani huku akitumia nafasi hiyo kutoa maelekezo na maagizo katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya kuhakikisha wananchi wanatunza vyanzo vya maji pamoja na miundombinu. Akizungumza leo na wananchi wa Kata ya Mwakitolyo mkoani Shinyanga, Chongolo amewapongeza wananchi hao kwa kuendelea kupata fedha kutoka serikalini kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji. “Ndugu zangu nimekuja hapa, nimepata nafasi ya kutembelea mradi wa ujenzi wa tanki la maji lililowekwa eneo ambalo wananchi watapata maji kwa asilimia 100.Hongereni na niwapongeze kwa kutunza eneo lile, “Nitoe mwito katika maeneo mengine wahakikishe wanatenga maeneo kwa ajili ya uhifadhi kwani yanatija sana, sio kila eneo anatakiwa kwenda ng’ombe , sio kila eneo linatakiwa kuchimbwa, sio kila eneo linatakiwa kutumiwa kwa kila kitu lazima muhifadhi kwa ajili ya matumizi maalum ndani ya maeneo yenu”. Akizungumza zaidi akiwa eneo hil

KISHINDO CHA MEMBE KUREJEA CCM,SHAKA AONGOZA MAPOKEZI.

Image
  Aliyewahi kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Bernard Membe ameeleza sababu zilizomfanya arejee CCM ikiwemo kuondoka kwa sababu ambayo ilimfanya atimkie upinzani. Aidha, amefungunguka jinsi alivyoumia kutokana na uamuzi wa kumwondolea uanachama wa CCM, Chama alichokulia huku akiahidi sasa atafia ndani ya CCM. Akizungumza katika mkutano huo, katika Kijiji cha Rondo, alisema Machi 30 hadi Aprili 1, mwaka huu aliitwa Dodoma, kwenye kikao cha kamati ya Maadili ya CCM Taifa na Vikao vya kamati kuu ya CCM na Halmashauri Kuu ambapo kote alipewa nafasi na Mwenyekiti wa CCM Taifa kuzungumza na wajumbe wa vikao hivyo juu ya kurejeshewa uanachama wake. “Mama yetu, Rais wetu na Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa Ndugu Samia Suluhu Hassan alinipa nafasi ya kuzungumza na wajumbe wa kamati kuu ya Chama Taifa. Nashukuru kwa kupewa nafasi ile na wajumbe waliliridhia kwa kauli moja nirejee CCM. Nimerejea CCM kwa sababu ku

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMATATU MEI 30, 2022

Image