PSSSF KATIKA MAONESHO YA BIASHARA NA UTALII TANGA
NA MWANDISHI WETU, TANGA MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) unashiriki katika maonesho ya bishara na utalii kwa kutoa elimu kwa wanachama kupitia maonesho yanayofanyika katika viwanja vya Mwahako jijini Tanga. PSSSF inashiriki katika maonesho haya pamoja na kutoa elimu kwa wanachama na wananchi wanaotembelea banda hilo, pia wanachama wanapatiwa huduma mbalimbali za kiofisi ikiwemo, kuangalia taarifa za michango ya wanachama, taarifa za malipo ya pensheni, uhakiki wa wanachama na kutoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya uanachama, alisema Bi. Rehema Mkamba, Afisa Mkuu wa Uhusiano, PSSSF Alisema ni fursa nzuri kwa Mfuko kukutana na wanachama wake lakini wananchi pia ambao watafika kwenye maonesho hayo maarufu kama Tanga Trade Fair ambayo yatadumu kwa siku 10 kuanzia Mei 28 hadi Juni 6, 2022. Wanachama wa PSSSF wakihidumiwa kwenye banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya biashara na utalii kwenye viwanja vya Mwahako jijini Tanga. Wananchi na wanachma