Posts

RAIS SAMIA AREJEA NYUMBANI AKITOKEA ZIARANI NCHINI MAREKANI

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wakati akitokea nchini Marekani tarehe 28 Aprili, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiagana na Makamu wa Rais Mhe. Philip Isdor Mpango mara baada ya kuhutubia Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha tarehe 28 Aprili, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa. Samia Suluhu Hassan akiagana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mara baada ya kuwahutubia Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro pamoja na Arusha katika uwanja wa Ndege wa KIA. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa. Samia Suluhu Hassan akiagana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mara baada ya kuwahutubia Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro pamoja na Arusha katika uwanja wa Ndege wa KIA. Kikundi cha ngoma za asili cha Kimasai kikitoa burudani mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu H

UFUATILIAJI NA TATHMINI WA MIPANGO YA MAENDELEO UPEWE KIPAUMBELE-MAJALIWA

Image
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema masuala ya ufuatiliaji na tathmini yanapaswa kupewa kipaumbele ili Taifa liendelee kupata matokeo yanayokusudiwa katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo. “Kwa kufanya hivyo, tutatoa nafasi ya kupima utendaji kwa ujumla na hivyo, kujua tumefikia wapi, tumekwama wapi na wapi tunahitaji kufanya maboresho. Lengo kuu ni kufikia malengo tarajiwa.” Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo  (Jumatano, Aprili 27, 2022) wakati akifungua Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Wiki ya Ufuatiliaji na Tathmini lililofanyika katika ukumbi wa PSSSF jijini Dodoma. Waziri Mkuu amesema kuwa kongamano hilo linaakisi maono na maelekezo ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu kuimarisha tasnia ya ufuatiliaji na tathmini. Waziri Mkuu amesema tayari Serikali imeandaa mwongozo wa ufuatiliaji na tathmini ya miradi na programu za maendeleo unaoainisha majukumu na wajibu wa kila mdau katika usimamizi wa miradi.  Amesema mwongozo

ANUANI ZA MAKAZI ZATOA FIRSA KWA VIJANA

Image
Na Immaculate Makilika – MAELEZO, Rukwa Mfumo wa Anwani za Makazi nchini unatajwa kuwa na fursa lukuki kwa vijana ikiwa ni pamoja na kubuni na kushiriki kutengeneza miundombinu kwa ajili ya mfumo huo nchini. Akizungumza leo mkoani Rukwa wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua na kuhamasisha utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi, Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Mhandisi, Kundo Mathew alisema kuwa Serikali imeendelea kutimiza dhamira yake ya kutoa fursa mbalimbali kwa Watanzania, ambapo    kupitia Mfumo wa Anwani za Makazi, vijana wenye ubunifu wamepata fursa ya kushiriki kutengeneza miundombinu kwa ajili ya Anwani za Makazi katika maeneo yao. Akitolea mfano mkoani Rukwa, Naibu Waziri huyo alisema “Nakupongeza sana Mkuu wa Mkoa kwa kushirikisha vijana hawa wazawa wa mkoa huu katika kazi hizi za kubuni na kutengeneza namba na vibao vinavyotumika katika zoezi hili ni dhahiri kuwa watapata kipato kwa utaalamu wao na wanafanyakazi hii k

TANZANIA NA MISRI ZAJADILI UTOZAJI KODI MARA MBILI

Image
  Na Benny Mwaipaja, Washington DC TANZANIA na Misri ziko katika hatua ya mwisho ya majadiliano ya kuipatia ufumbuzi changamoto ya utozaji kodi mara mbili kwenye bidhaa zinazoingia au kutoka katika nchi hizo mbili ili kusisimua biashara na kukuza mauzo nje ya nchi yatakayoongeza upatikanaji wa fedha za kigeni. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Dkt. Rania Al-Mashat, kando ya mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa- IMF, Jijini Washington DC, Marekani. Bw. Tutuba alisema kuwa majadiliano ya wataalam wa masuala ya kodi kutoka pande zote mbili yanaendelea na kuahidi kuwa ndani ya kipindi cha miezi miwili yatakuwa yamekamilika na kuwashauri viongozi wa juu wa nchi kuhusu hatua zilizofikiwa ili kuondoa changamoto hiyo kwa lengo la kuboresha biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Misri. Kuhusu uwekezaji na ukuzaji biashara, Bw. Tutuba alimh

KUTOKA MAGAZETINI LEO ALHAMISI APRILI 28, 2022

Image
 

PSSSF YAPONGEZA JITIHADA ZA RAIS SAMIA KUIFUNGUA NCHI, WAPANGAJI KWENYE MAJENGO YAKE YA VITEGA UCHUMI WAONGEZEKA

Image
  NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), C.P.A Hosea Kashimba amesema kuongezeka kwa idadi ya wapangaji kwenye jengo jipya na la kisasa la Kitega Uchumi la PSSSF Commercial Complex lililoko barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es Salaam, ni matokeo ya jitihada kubwa anazofanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan za kufungua nchi pamoja na kuweka mazingira mazuri ya kufanya kibiashara. C.P.A Kashimba ameyasema hayo Aprili 27, 2022 wakati wa hafla ya utiaji saini wa Mkataba wa upangishaji kwenye jengo hilo kati ya Mfuko na Kampuni ya MIC Tanzania PLC wamiliki wa Mtandao wa simu, Tigo katika hafla iliyofanyika kwenye jengo hilo. “Kampuni ya Tigo kuamua kuyaweka Makao yake Makuu hapa ni heshima kubwa sana kwetu, lakini pia idadi ya wapangaji kwenye jengo letu imeongezeka na hivi karibuni tunategemea nafasi nyingi zaidi za jengo kujazwa kwakuwa tumeshasaini mikataba ya upangishaji na taasisi kadha