PROF. MBARAWA ATOA MIEZI MITATU UKARABATI MV. KAZI
WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amemtaka mkandarasi Songoro Marine anayefanya ukarabati mkubwa wa Kivuko cha MV. Kazi kuhakikisha kivuko hicho kinakamilika ndani ya kipindi cha miezi mitatu kuanzia sasa. Akizungumza alipokagua ukarabati wa kivuko hicho leo jijini Dar es Salaam, Prof. Mbarawa amesema Serikali imeshapata fedha kwa ajili ya ukarabati huo, hivyo ni wajibu wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) na Mkandarasi Songoro Marine kuhakikisha taratibu za manunuzi na mikataba ya kazi hiyo inakamilika kwa haraka. "...Hakikisheni ifikapo Ijumaa ya Aprili Mosi taratibu za mikataba ziwe zimekamilika na kasi ya ujenzi na uagizaji vifaa nje ya nchi kwa ajili ya kazi hiyo iongezeke ili kufikia lengo," amesisitiza Prof. Mbarawa. Prof. Mbarawa amesema idadi ya wakazi wa Kigamboni wanaohitaji huduma ya kivuko imekuwa ikiongezeka siku hadi siku hivyo kuwataka TEMESA kutengeneza ratiba maalum ya ukarabati wa vivuko vyake ili kuondoa usumbufu pindi v