Posts

KUTOKA MAGAZETINI LEO IJUMAA FEB 25, 2022

Image
 

WIZARA YA AFYA YAKABIDHI MASHINE ZA KISASA ZA KUCHANGANYA CHUMVI NA MADINI JOTO.

Image
 Na WAF- DOM.  Wizara ya Afya imekabidhi mashine tano za kisasa za kuchanganya chumvi na madini joto kwa Ofisi ya Rais-TAMISEMI zilizotolewa na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kupitia shirika la Kimataifa la Nutrition International kwa ajili ya kusimikwa katika Mikoa ya Tanga, Pwani na Mtwara itayosaidia kuongeza uzalishaji wa chumvi yenye kiwango cha  kutosha cha madini joto nchini.  Akizungumza wakati wa kukabidhi mashine hizo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi amesema Utafiti uliofanyika nchini mwaka 2019 ulibaini Tanzania inazalisha chumvi Tani 330,712 kwa mwaka na kati ya Chumvi hiyo Tani 141,228 ambapo ni sawa na asilimia 43 haiwekwi madini joto hivyo ujio wa mashine hizo utasaidia kuongeza uzalishaji wa chumvi yenye madini hayo. Prof. Makubi amesema mashine hizo ambazo zimetengenezwa nchini na Wataalamu kutoka VETA zimeweza kugharimu kiasi cha shilingi milioni 55 huku gharama ya mashine moja ikigharamu kiasi cha shilingi mil

MAENDELEO YA VIWANDA YAENDE SAMBAMBA NA UHIFADHI MAZINGIRA: DKT. JAFO

Image
Serikali imesema kamwe haitakuwa kikwazo kwa wawekezaji wanaolenga kuwekeza katika sekta ya viwanda bali maendeleo ya viwanda ni lazima yaende sambamba na hifadhi ya Mazingira. Rai hii imetolewa leo Februari 24, 2022 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Dkt. Selemani Jafo katika ziara ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira katika Kiwanda cha A One product and Bottles Ltd katika Mkoa wa Dar es Salaam. Dkt. Jafo amesema Serikali inahimiza wawekezaji nchini lakini ni vema wawekezaji hao wazingatie Sheria ya Usimamizi wa Mazingira kwa ukamilifu wake. Katika ziara ya kukagua kiwanda hicho kinachozalisha vinywaji baridi (soda, maji na juisi).  Waziri Jafo amepongeza utii wa Kiwanda hicho kwa kutekeleza kwa wakati maagizo ya Serikali ya kutotumia karatasi za plastiki kwenye vifuniko vya chupa za maji. “Kiwanda hiki kimenifurahisha sana, wametii kwa vitendo maagizo ya Serikali ya kutotumia karatasi za plastiki kwenye vifuniko vya chupa za maji y

WAZIRI MKUU MAJALIWA AMUWAKILISHA RAIS SAMIA MKUTANO WA ROM NCHINI CONGO DRC

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameshiriki kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan mkutano wa kumi wa wakuu wa nchi wa Serikali zinazohusika na mpango wa Amani, Usalama na Ushirikiano nchini DRC na kwenye ukanda wa maziwa makuu unaofanyika leo, Februari 24, 2022 jijini Kinshasa, DR C  

SPIKA DKT. TULIA ACKSON ASHIRIKI SEMINA YA MAFUNZO KWA WABUNGE

Image
  Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akiwa na Naibu wake, Mhe. Mussa Azzan Zungu ameshiriki semina ya mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo Wajumbe wa Kamati ya Uongozi, Makamu Wenyeviti wa kamati na Tume ya Utumishi wa Bunge ambayo yanaendelea katika Ofisi ndogo za Bunge zilizopo Tunguu, Zanzibar.

MAPOKEZI MAKUBWA YAMSUBIRI SPIKA WA BUNGE DKT. TULIA ACKSON JIJINI MBEYA

Image
 Na mwandishi wetu, Mbeya. Wananchi jijini Mbeya wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini, kupitia Chama  Cha  Mapinduzi (CCM) Dkt.Tulia Ackson Mwanasansu ambaye hivi karibuni alichaguliwa kuwa spika wa bunge  la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Kauli hiyo imetolewa leo Februari 24, 2022, na katibu mwenezi  wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya mbeya Bw. Philimon Mng’ong’o wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kumpokea mbunge huyo ambaye mara hii anarudi akiwa na heshima ya uspika wa bunge. “Tarehe 26 mwezi huu siku ya jumamosi,chama cha mapinduzi CCM,Mbeya mjini kitakuwa na mapokezi ya spika wa bunge,mapokezi haya yataanzia eneo la Nsalaga kuanzia saa tatu asubuhi hivyo tunawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi katika viwanja vya Ruandanzovwe kwani kutakuwa na burudani mbalimbali za asili huku msanii wa kizazi kipya Rayvany akitarajiwa kutumbuiza kabla ya spika kuwahutubia wanananchi wa Mbeya’’Amesema Mng’ong’o. Ameong

WAZIRI MKUU MAJALIWA YUKO CONGO DRC KUHUDHURIA MKUTANO WA AMANI, USALAMA NA USHIRIKIANO NCHINI HUMO

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Congo DRC, Luteni Jenerali Paul Mella (katikati baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nd’jili jijini Kinshasa DRC kwa ajili ya kushiriki mkutano wa kumi wa Wakuu wa nchi wa Serikali zinazohusika na mpango wa Amani, Usalama na Ushirikiano nchini DRC na kwenye ukanda wa Maziwa Makuu. Mkutano huo unaanza leo Februari 24, 2022. kushoto ni Balozi wa Congo Nchini Tanzania Mhe. Jean Pierre Mutamba  

JK ARIDHISHWA NA DHAMIRA YA SERIKALI KWENYE SEKTA YA MADINI

Image
  RAIS mstaafu wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Dkt.Jakaya Kikwete amesema kuwa, kauli mbiu ya mwaka huu katika Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Uwekezaji Katika Sekta ya Madini inadhirisha nia ya Serikali ya kuifanya Sekta ya Madini iweze kutoa mchango unaostahili kwa Taifa. Kauli mbiu hiyo ya "Mazingira Wezeshi kwa Maendeleo ya Sekta ya Madini" ilikuwa inaongoza mkutano huo wa siku mbili ambao ulifanyika kati ya Februari 22 hadi 23, 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere kilichopo jijini Dar es Salaam. Dkt. Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla maalum ya Usiku wa Madini uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam amesema kuwa, kauli mbiu hiyo inaonesha dhamira ya kuiwezesha Sekta ya Madini itoe mchango stahiki kwa maendeleo ya Taifa letu tofauti na miaka ya nyuma. "Pia inahakisi azma ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mama yetu mpendwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kusimamia mabadiliko ya kiser