Posts

ORODHA YA WALIOOMBA KAZI TAKUKURU: WAITWA KWA USAILI

Image
Orodha Ya Walioitwa Kwenye ... by Ummy Kupata orodha kamili bofya hapa> https://www.pccb.go.tz/index.php/sw/265-nafasi-za-kazi/719-maombi-ya-kazi  

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMATANO DISEMBA 29, 2021

Image
 

RAIS SAMIA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI RELI YA SGR MAKUTUPORA-TABORA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia kwenye Hafla ya utiaji saini Mkataba wa mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha kutoka Makutupora (Singida) hadi Tabora Chenye urefu wa kilomita 368 katika awamu ya tatu ya mradi huo (Lot III) Hafla hiyo imefanyika leo tarehe 28 Desemba 2021 Ikulu Jijini Dar es salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishuhudia utiaji Saini Mkataba wa mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha kutoka Makutupora (Singida) hadi Tabora chenye urefu wa Kilometa 368 katika kipande cha tatu cha mradi huo (Lot III). Wa kwanza (kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu Shirika la Reli nchini (TRC) Bw. Masanja Kadogosa akiweka saini moja ya Kitabu cha Mkataba huo pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Yapi Merkez ya Uturuki Bw. Erdem Arioglu katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 28 Desemba 2021. Mkurugenzi Mkuu Shirika la Reli nchini Bw. Masanja Kadogosa pamoja na M

MUFTI AWAASA WATANZANIA

Image
  Mufti Mkuu wa Tanzania shehe Abubakari Zuberi amewatahadharisha watanzania kuilinda amani ya nchi yetu kwamba ikiondoka kuirudisha itachukua muda mrefu. Amesema hayo katika Maulidi ya kumswalia mtume iliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mkuranga Wilayani Mkuranga mkoani Pwani nakuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini ya kiislam kutoka nchi za uarabuni, Uingereza, Lamu mjini Mombasa nchini Kenya, mashehe kutoka mikoa ya Dar es salaam na uongozi wa Bakwata mkoa wa Pwani na wilaya ya Mkuranga sambamba na uongozi wa chama na serikali ngazi ya wilaya ya Mkuranga. Amesema amani iliyopo katika nchi yetu ikiondoka inaweza kuchukua hata miaka 50 kurudi tena katika nchi yetu na kwamba wengi wetu inawezekana hatutakuwepo kipindi hicho. "Amani tuliyonayo tukiichezea ikatoweka na ikitoweka hairudi mapema inaweza kuchukua miaka mingi hata miaka 50 sisi sote tunaweza tukawa hatupo kipindi hicho Kwa sababu kitu tunacho tunakichezea kama vile amani" Mufti Mkuu Shehe Abubakari

RAIS MWINYI AWAAPISHA WAJUMBE WAPYA TUME YA MIPANGO ZANZIBAR

Image
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, kuwa Mjumbe mpya wa Tume ya Mipango, hafla hiyo iliyofanyika leo 27-12-2021, katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar. RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mwanasheria Mkuu Mhe.Dkt. Mwinyi Talib Haji, kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango, hafla hiyo iliyofanyika leo 27-12-2021, katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar. RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar.Mhe Jamal Kassim Ali,kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango,hafla hiyo iliyofanyika leo 27-12-2021, katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisaini hati ya Kiapo ya Waziri wa Ardhi, Maendeleo na Makaazi Zanzibar Mhe.Riziki Pembe Juma, baada

RAIS SAMIA ATOA ZAIDI YA BILIONI 12 KUPUNGUZA KERO YA MAJI MKOANI SINGIDA

Image
   Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Singida Mhandisi Lucas Japhary (kushoto) na Mhandisi na Mkurugenzi wa Mashauri T.C.L, Jonas Mwazyunga wakisaini mkataba  kwa jili ya ujenzi wa mradi wa Milade na Kaserya wenye gharama ya Sh.818,601,228 katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki. Mkuu wa Mkoa  Singida Dkt. Binilith Mahenge akishuhudia utiaji wa saini wa mikataba hiyo Mkuu wa Mkoa     Singida Dkt. Binilith Mahenge akizungumza baada ya kushuhudia utiaji wa saini wa mikataba hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida  Juma Kilimba. Watendaji wa RUWASA wakiwatayari kushiriki kutia saini mikataba hiyo na Wakandarasi. Mmoja wa wakandarasi hao akijitambulisha. Mkurugenzi wa kampuni ya Chakware Mhandisi Bagambo Bakari akishukuru kupata ujenzi wa mradi wa maji wilayani Ikungi na Manyoni wenye thamani ya Sh.4.9 Milioni. Mkandarasi kutoka Mwanza akishukuru kupata kazi ya ujenzi wa mradi wa maji katika Wilaya ya Ikungi ambao u