Posts

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMANNE DISEMBA 28, 2021

Image
 

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMATATU DISEMBA 27, 2021

Image
 

DESMOND TUTU AFARIKI DUNIA

Image
Askofu Mkuu Mstafu wa Afrika Kusini, Desmond Tutu amefariki dunia Leo Disemba 26, 2021 akiwa na umri wa miaka 90, Ikulu ya nchi hiyo imethibitisha. Tutu ambaye ni Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya mwaka 1984, kwa kuendesha upinzqni dhidi ya Utawala wa kibaguzi wa makaburu wa Afrika Kusini bila ya kutumia nguvu, kwa muda mrefu alikuwa akisumbuliwa na maradhi. Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa amesema kifo chake ni pigo lingine kwa kuondokewa na kizazi cha wapigania ukombozi wa Afrika Kusini.

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAPILI DISEMBA 26, 2021

Image
 

MAKAMU WA RAIS AUNGANA NA WAUMINI WA KIKRISTO KATIKA IBADA YA MISA TAKATIFU YA KUZALIWA YESU KRISTO

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwa na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango leo tarehe 25 desemba 2021 wameungana na waumini wa kanisa katoliki la mtakatifu Paulo wa Msalaba Jimbo Kuu la Dodoma kushiriki ibada ya misa takatifu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo (Krismasi) misa ilioongozwa na Padri Julius Soteri. Desemba 25,2021.  

KAMANDA WA POLISI MKOANI IRINGA AFANYA OPARESHENI BARABARA KUU IRINGA -MOROGORO

Image
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan L. Bukumbi akiambatana na Mkuu wa Usalama Barabarani wamefanya Operesheni katika barabara kuu ya Morogoro - Iringa hususani eneo la Kitonga lakini pia kutoa elimu kwa Madereva ili kuepusha ajali zinazoweza kuzuilika hasa kipindi hiki cha Sikukuu za Mwisho wa Mwaka. ACP Bukumbi amewakumbusha madereva kutii sheria za barabarani ili kuepuka ajali na kwamba hatosita kumchukulia hatua dereva yeyote atakaekiuka maadili ya udereva awapo barabarani. Hali kadhalika Mkuu wa Usalama barabarani Mkoa wa Iringa, SP Yusuf Kamota ametumia muda huo kuwakumbusha kuwa Iringa sio sehemu sahihi kwa madereva wasiofuata sheria za barabarani na kwamba atahakikisha sheria zinatekelezwa ipasavyo. Katika hatua nyingine, Kamanda Bukumbi amewataka abiria wawapo safarini, kutoa taarifa kwa wakuu wa usalama barabarani endapo kuna vitendo vya uvunjifu wa sheria kwani Jeshi la Polisi limeweka utaratibu wa kubandika mawasiliano kwenye Vyombo hivyo.