Posts

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAMOSI NOVEMBA 26, 2021

Image
 

JULIUS NGUHULA MBOBEZI WA MASUALA YA USAFIRI WA MELI AZINDUA KITABU KINACHOELEZEA HATUA MUHIMU ZA KUSAFIRISHA MIZIGO

Image
  Mtanzania mbobezi katika tasnia ya usafirishaji mizigo kwa meli Julius Nguhula aliyetunga kitabu cha (Enhancing your Knowledge in Shipping) ambacho kimeeleza hatua kwa hatua mchakato wa kuagiza na kusafirisha mizigo kwa usafiri wa meli. akiwa na Mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro Dk.Charles Kimei wa pili kutoka kushoto, Mh.David Kihenzile mbunge wa  Jimbo la Mufindi Kusini na mwenyekiti wa Bunge kushoto pamona ja Emmanuel Malya Mwenyekiti wa Kampuni ya Maritine Group wakipiga makofi mara baada ya kuzinduliwa kwa kitabu hicho leo kwenye hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es Salaam.  ............................................ WADAU wa sekta ya usafirishaji kwa njia ya meli wamekutana jijini Dar es Salaam kushuhudia uzinduzi wa kitabu cha Enhancing your Knowledge in Shipping ambacho kimeeleza hatua kwa hatua mchakato wa kuagiza na kusafirisha mizigo kwa usafiri wa meli. Kitabu hicho ambacho ni cha kwanza kabisa kuandikwa katika tasnia ya usafirishaji mizigo kw

KUTOKA MAGAZETINI LEO ALHAMISI NOVEMBA 25, 2021

Image
 

ANDAENI PROGRAM ZA UKUZAJI AJIRA-MAJALIWA

Image
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameziagiza wizara zote zenye dhamana ya ukuzaji ajira kuhakikisha zinaandaa programu na mikakati bora ya ukuzaji ajira ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wadau wote nchini washiriki katika utekelezaji wake ili kukabiliana na changamoto za ukosefu wa ajira. Pia, Mheshimiwa Majaliwa amezielekeza Ofisi na Wizara zote zenye dhamana za uwekezaji na biashara zihakikishe zinashirikiana na wadau wengine hususan sekta binafsi kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kutoa fursa ya kuanzishwa kwa viwanda vitakazochochea ukuaji wa uchumi na kuongeza ajira.  ametoa maagizo hayo leo (Jumatano, Novemba 24, 2021) wakati akizindua Matokeo ya Viashiria Muhimu vya Soko la Ajira kutokana na utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka 2020/2021. Uzinduzi huo umefanyika katika Hotel ya Golden Tulip, Zanzibar. Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa idadi ya watu walio na ajira nchini imeongezeka kutoka watu milioni 20.5 mwaka 2014 hadi kufikia watu milioni 24.1 mwaka 2020

NHC YATAKIWA KUENDELEA KUWEKEZA KATIKA MIRADI YA KIMKAKATI

Image
Na   Munir Shemweta, MISENYI Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuendelea kuwekeza miradi ya kimkakati itakayoliwezesha shirika kujiongezea kipato. Dkt Mabula ametoa kauli hiyo tarehe 23 Novemba 2021 wakati akikagua mradi wa jengo la kibiashara la NHC lilipo mpakani mwa Tanzania na Uganda eneo la Mutukula wilaya ya Misenyi mkoani Kagera. Naibu Waziri ambaye alikuwa katika  ziara ya siku mbili mkoani Kagera alisema, ilichofanya NHC kujenga jengo la kibiashara katika mpaka wa Tanzania na Uganda Mutukula ndicho serikali inachokitaka pale inapokuwa na taasisi zinazojitegemea katika uendeshaji pia ziwe na njia tofauti za kujiongezea kipato kitakachosaidia kuongeza miradi mingine.  " Hiki ambacho NHC mmekifanya hapa kujenga jengo la biashara Mutukula ndicho inachokitaka serikali  kuwa inapokuwa na taasisi inayojitegemea kiuendeshaji pia iwe na njia tofauti za kujiongezea kipato cha shirika " alisema Dkt Mabula. Kwa mujibu