WIZARA YAONGEZA NGUVU KUDHIBITI UTOROSHAJI MAZAO YA UVUVI
Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi Bw. Emmanuel Bulayi (kushoto), akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah (katikati) juu ya utendaji kazi wa injini tano za kupachika kwenye boti zilizonunuliwa na idara hiyo kwa ajili ya vituo vya ulinzi na usimamizi wa rasilimali za uvuvi Kanda ya Ziwa Victoria. Hafla hiyo fupi imefanyika katika ofisi za wizara hiyo zilizopo Mtumba jijini Dodoma. Aliye upande wa kushoto kwa katibu mkuu ni Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbemaji Dkt. Nazael Madalla. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - Wizara ya Mifugo na Uvuvi). Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah (kulia) akimkabidhi injini ya kupachika kwenye boti Afisa Mfawidhi Kituo cha Ulinzi na Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi Kanda ya Mwanza Bw. Gabriel Mageni na kuwataka maafisa wafawidhi kuhakikisha wanatumia vifaa hivyo kwa ajili ya kudhibiti utoroshaji wa mazao ya uvuvi kwenda nchi za j