WAZIRI NDAKI ANG’AKA UKUSANYAJI MDOGO WA MADUHULI
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (Mb) akizungumza wakati wa kupokea taarifa ya ukusanyaji wa maduhuli ya robo mwaka kwa bajeti ya wizara ya mwaka wa fedha 2021/22 Sekta ya Mifugo jijini Dodoma, ambapo Waziri Ndaki amesema utaratibu wa ukusanyaji maduhuli uko wazi lakini kuna shida ya namna ya ukusanyaji pamoja na fedha nyingine kutojulikana zinapopelekwa baada ya kukusanywa. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - Wizara ya Mifugo na Uvuvi). Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) akizungumzia kukerwa na utoroshaji wa rasilimali za mifugo nchini kwenda nje ya nchi na uingizaji wa mazao ya mifugo kinyume na utaratibu ambapo wanaweza kuwa wanaingiza mazao mbalimbali kwa kuwa hawalipi kodi na kuathiri uzalishaji ndani ya nchi mambo ambayo hayavumiliki. Amezungumza hayo wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya ukusanyaji wa maduhuli ya robo mwaka kwa bajeti ya wizara ya mwaka wa fedha 2021/22 Sekta ya Mifugo jijini Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasil