MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA BENKI YA DUNIA DKT. GHANEM
Makamu wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango hii leo Septamba 28, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt Hafez Ghanem Ikulu Chamwino mkoani Dodoma. Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Rais Dkt. Mpango amemuhakikishia Dkt. Ghanem kwamba Tanzania itaendelea kushirikiana na Benki hiyo katika masuala mbalimbali ya kuinua uchumi hapa nchini. Makamu wa Rais Dkt. Mpango amesema kwamba serikali ya awamu ya sita imeweka kipaumbele katika kuinua sekta binafsi pamoja na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji hapa nchini. Amesema mpango wa maendeleo wa miaka mitano umelenga kuinua sekta ya viwanda hapa nchini hivyo serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kufanikisha hilo. Aidha Makamu wa Rais Dkt. Mpango amesema ili kukidhi mahitaji ya sekta binafsi hapa nchini serikali imeweka mkazo katika sekta ya elimu hasa elimu ya ufundi ili kupata wahitimu wenye ujuzi watakaoweza kusaidia kuinua sekta hiyo. Makamu wa R