DC MOYO:WAKURUGENZI WATAKAOKAIDI MAAGIZO YA LISHE KUCHUKULIWA HATU KALI ZA KIDHAMU.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akizungumza kwenye kikao kazi na wanawake vinara wa lishe bora namna ya kutafuta njia ya kutatua tatizo la udumavu mkoani Iringa Baadhi ya wanawake vinara wa lishe bora wakiwa makini kumsikiliza meneja wa shirika lisilo la kiserikali la Save the Chidren mkoani Iringa John Masenza wakati semina ya kukabiliana na udumavu mkoani Iringa. Na Fredy Mgunda,Iringa. Mkoa wa Iringa umeziagiza halmashauri zote kuhakikisha zinatenga na kutoa fedha kwa ajili ya kupambana na tatizo la udumavu ambalo limekuwa linaleta doa licha ya mkoa huo kuwa mmoja ya mikoa ambayo inaongoza kwa kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula. Akizungumza kwenye mkutano na wanawake vinara wa halmashauri tatu za mkoa huo,mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Iringa alisema kuwa kumekuwa na changamoto ya utolewa wa fedha kutoka kwa wakuu wa Idara mbalimbali za Halmashauri na kukwamisha mpango wa serikali ya mkoa kukabiliana natatizo la udum