Posts

MBUNGE NEEMA LUGANGIRA ATOA NENO FEDHA ZINAZOKUJA NCHINI KWA AJILI YA NGOs

Image
MBUNGE wa Viti Maalumu CCM (NGOs Tanzania Bara) Neema Lugangira akizungumza  wakati wa  Uzinduzi wa Wiki ya Azaki imefanyika Jijini Dar es Salaam Julai 29 Julai 2021 MBUNGE wa Viti Maalumu CCM (NGOs Tanzania Bara) Neema Lugangira amesema umesema wakati kuhakikisha fedha za ufadhili ambazo zinatoka nje ya nchi zinazokuja nchini ziweze kufanyiwa kazi na kutelezwa na NGOs na CSOs kutoka ndani ya nchi, Aliyasema hayo Siku ya Uzinduzi wa Wiki ya Azaki imefanyika Jijini Dar es Salaam Julai 29 Julai 2021 ambapo alisema takwimu zinaonyesha kwamba zile fedha ambazo zinazoingia kwa ajili ya Sekta ya Azaki ni asilimia 1 pekee yake ndio zinaekwenda kwa CSOs, NGOs ambazo zimeanzishwa na Watanzania. Mbunge Lugangira alisema kwa sababu takwimu zinaonyesha asilimia 99 ya fedha zinazotoka nje zinapita kupitia mashirika ambazo sio ya kiserikali lakini ni ya Kimataifa huku akieleza ili miradi yetu iwe endelevu lazima NGOs/CSOs za ndani ziweze kushiriki katika utekelezaji wa miradi hiyo na ndio ma

MHANDISI MASAUNI ARIDHISHWA NA UTENDAJI WA SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA

Image
Msaada wenu tafadhali Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, amelipongeza Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwa kuongeza ufani na kuboresha utendaji kazi wa Shirika hilo na kufanikiwa kuongeza kiwango cha uwekezaji kutoka sh. bilioni 85 mwaka 2018/2019 hadi kufikia shilingi bilioni 245 Mwaka 2020/2021. Mhandisi Masauni ametoa pongezi hizo  alipotembelea Makao Makuu ya Shirika la Bima la Taifa Jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya Shirika hilo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea Taasisi zote zilizochini ya Wizara ya Fedha na Mipango, baada ya kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo. “Moja ya eneo lililonivutia ni namna Shirika hili lilivyoboresha huduma zake na  mapato kwa kutumia mifumo ya TEHAMA, kutoka asilimia 10 za miaka ya nyuma hadi kufikia asilimia 95 katika kipindi cha miaka miwili tu iliyopita” Alisema Mhe. Masauni Ameuagiza uongozi wa Shirika hilo kuongeza ubunifu na bidii zaidi

RAIS SAMIA APOKEA NDEGE MPYA AINA YA BOMBADIER DASH 8-Q400 ILIYONUNULIWA NA SERIKALI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa pamoja na Viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria kupokea Ndege Mpya aina ya Bombadier DASH 8-Q400 iliyonunuliwa na Serikali ya Tanzania na kukodishwa kwa  Shirika la Ndege la ATCL ilipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 30  Julai, 2021. Wa pili kushoto ni Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango na wa tatu kulia ni waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasalimia Wananchi waliofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya kumuunga Mkono kwenye mapokezi ya Ndege Mpya aina ya Bombadier DASH 8-Q400 iliyonunuliwa na Serikali ya Tanzania na kukodishwa kwa  Shirika la Ndege la ATCL ilipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 30  Julai, 2021. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoka

USIKIVU WA TBC WAPANDA KWA ASILIMIA 14 NDANI YA MIEZI MIWILI

Image
    Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Innocent Bashungwa(Mb), na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe.Dkt. Faustine Ndungulile (Mb);wakikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Kituo cha kurushia matangazo ya Redio ya TBC eneo la Kisaki - Morogoro leo Julai, 2021. Mtaalam wa Mitambo akitoa maelezo kwa  viongozi  mbalimbali waliohudhuria  kwenye  ya uzinduzi wa Kituo cha kurushia matangazo ya Redio ya TBC eneo la Kisaki - Morogoro leo Julai, 2021. Na John Mapepele, WHUSM Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe Innocent Bashungwa amesema hadi kufikia Mwezi Septemba, mwaka huu usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) utapanda kuzifikia Wilaya 120 sawa na 76% kutoka Wilaya 103 ambapo ni sawa na 64% za usikivu wa sasa ili kuhahakikisha wananchi wote wanapata habari kwa uhakika. Mhe. Bashungwa ameyasema hayo leo Julai 30, 2021 kwenye uzinduzi wa kituo cha kurushia matangazo ya redio eneo la Kisaki mkoani Morogoro ambapo amesema katika Bajeti

SERIKALI ITAHAKIKISHA ZAO LA MKONGE LINAIMARIKA-RC MALIMA

Image
   Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua ukarabati wa Mashine za kuchakata mkonge ambapo awali zilikua chakavu hali iliyokua ikisababisha kushuka kwa uzalishaji wa zao la Mkonge. Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) Balozi Alli Siwa akizungumza Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sisalana Elizaberth Kalambo akielezea jambo Sehemu ya wananchi wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima NA OSCAR ASSENGA, KOROGWE SERIKALI Mkoani Tanga imesema itahakikisha zao la Mkonge linaimarika kutokana na ongezeko la mahitaji ya bidhaa zitokanazo na zao hilo duniani yanayolenga kuachana na matumizi ya bidhaa za Plastiki ambazo zina athari kwa Jamii.  Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima wakati wa ziara yake ya kukagua ukarabati wa Mashine za kuchakata mkonge ambapo awali zilikua chakavu hali iliyokua ikisababisha kushuka kwa uzalishaji wa zao la Mkonge.  Mkuu huyo wa mkoa alisema kwa

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAMOSI JULAI 31, 2021

Image
 

RC KUNENGE AWAONGOZA WANANCHI MKOA WA PWANI KUCHANJA CHANJO DHIDI YA UVIKO 19 MJINI KIBAHA

Image
 MKUU wa mkoa wa Pwani,  Mhe. Abubakar Kunenge, amepata chanjo ya UVIKO 19 leo Julai, 30 2021. Akichanjwa chanjo hiyo katikà viwanja vya kituo cha Afya Mkoani, kilichoko Kibaha Mjini, Mhe. Kunenge amewaasa Wanachi wa Mkoa huo kuwa ugonjwa upo na kuwataka kuchukua tahadhari wakati wote, amewataka Kuvaa barako, kunawa mikono kwa maji tiririka na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima. Amemshukuru Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuonyesha njia kwa kupata chanjo. "nimechanja kwa hiari yangu mwenyewe mpaka sasa najisikia vizuri sijaona shida yeyote," alisema RC KUNENGE na kuongeza...... Wananchi waje wachanje kwa hiari yao tunachotafuta ni salama tumepata chanjo kidogo tunaendelea kuratibu upatikanaji wa nyingi zaidi na tutaitoa bila usumbufu na bila malipo. "Chanjo hii kwa sasa itatolewa kwa makundi ya Kipaumbele kama vile watoa huduma ya afya, watu wenye umri kuanzia miaka 50 na kuendelea kama ambavyo muongozi wa Wizara ya Afya kuhusu Chanjo hiyo unavyosema. Mkuu wa Mkoa wa P