Posts

NAIBU WAZIRI GEKUL ATAKA UPANUZI WA KITUO CHA KIMATAIFA CHA MICHEZO MALYA UKAMILIKE SEPTEMBA

Image
a.     Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul akipata maelezo juu ya maendeleo ya ujenzi wa hosteli ya Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kutoka kwa Mkuu wa Chuo Richard Mganga alipotembelea eneo hilo Julai 17, 2021. Nyuma ni Mkururugenzi Msaidizi wa Michezo Addo Komba, kulia Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Samizi. a.     Mafundi wakiendelea kufyatua matofali kwa ajili ya kujengea hosteli ya Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya itakayokuwa na uwezo wa kuchukua zaidi ya wanachuo 190. a.     Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul akihutubia kwenye mahafali ya kumi (10) ya Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya Julai 17, 2021. a.     Wanachuo wa chuo cha Michezo Malya waonyesha mchezo wa kufanya mazoezi kwenye mahafali ya kumi (10) ya Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya Julai 17, 2021 Na John Mapepele, Mwanza Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul ameutaka Uongozi wa Chuo c

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.HUSSEIN ALI MWINYI AMEZINDUA NA KUSHIRIKI MASHINDAO YA RIADHA YA KIMATAIFA YA ZANZIBAR INTERNATIONAL MARATHON

Image
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akishiriki katika Mbio za Marathon za Kilomita 5 zilizoazia katika viwanja vya Ngome Kongwe Jijini Zanzibar na kumalizia katika Uwanja wa Amaan na (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kulia kwa Rais) Kaimu Afisa Mkuu Ukaguzi wa Ndani wa Benki ya NMB Ndg.Benedicto Baragomwa. wakishiriki katika Mashindano ya Kimataifa ya Riadha ya Zanzibar International Marathon.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipiga bastola juu kuzindua Mashindano ya Riadha ya Kimataifa ya  Zanzibar International Marathon ya kilomita  5, yalioazia katika eneo la Ngome Kongwe Jijini Zanzibar na kumalizia katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar(Picha na Ikulu) BALOZI Mdogo wa Jamhuri ya Watu wa China anayefanyia kazi zake Zanzibar Mhe. Zhang Zhisheng akishiriki mbio za Zanzibar International Marathon za Kilimomita  5 (kulia kwake) na Mdau wa Michezo Z

NAIBU WAZIRI MABULA APIGA MARUFUKU WANAOSHITAKIANA MABARAZA YA ARDHI KUGHARAMIA USAFIRI

Image
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimpatia Kompyuta Afisa Ardhi Mteule wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma mkoa wa Songwe James Francis kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa shughuli za ardhi katika halmashauri hiyo wakati wa uzinduzi Baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya katika mkoa wa Songwe jan Na Munir Shemweta, SONGWE Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amepiga marufuku wananchi wanaoshitakiana kwenye Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya kugharamia usafiri wa kwenda uwandani wakati wa kusikiliza mashauri ya ardhi. Akizungumza wakati wa kuzindua Baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya, mkoa wa Songwe jana  Dkt Mabula alisema, asingependa kuona wananchi  wanaoshitakiana katika kesi ya ardhi mmoja wao atoe fadhila ya usafiri wa kwenda uwandani. ‘Tusingependa wale wanaoshitakiana mmoja wao atoe fadhila ya usafiri maana baada ya hapo mara nyingi wazee wa Baraza wanashawishika na kuona anayetoa usafiri kuwa amekuwa ni msamamaria mwema kwa

RAIS SAMIA AMALIZA ZIARA YAKE NCHINI BURUNDI, AREJEA NCHINI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili wakati akitokea nchini Burundi leo tarehe 17 Julai, 2021 baada ya ziara yake ya siku mbili nchini humo. PICHA NA IKULU   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Viongozi mbalimali wa Serikali ya Burundi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Melchior Ndadaye  Jijini Bujumbura Burundi baada ya kukamilisha ziara yake ya Kitaifa ya siku mbili Nchini Burundi leo Julai 17,2021. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Rais wa Jamhuri ya Burundi  Mhe. Evariste Ndayishimiye kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Melchior Ndadaye  Jijini Bujumbura Burundi baada ya kukamilisha ziara yake ya Kitaifa ya siku mbili Nchini Burundi leo Julai 17,2021. (Picha na Ikulu)

RAIS SAMIA AHUTUBIA JUKWAA LA WAFANYA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA BURUNDI

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye wakiingia katika Ukumbi wa Royal Jijini Bujumbura Burundi kwa ajili ya kuhutubia katika Jukwa la Wafanyabiashara wa Tanzania na Burundi lililofanyika leo Julai 17,2021. Ambapo Mhe. Rais Samia amekamilisha ziara yake ya siku mbili Nchini Burundi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye wakipokea heshima ya wimbo wa Taifa walipowasili katika Ukumbi wa Royal Jijini Bujumbura kwa ajili ya kuhutubia katika Jukwa la Wafanyabiashara wa Tanzania na Burundi lililofanyika leo Julai 17,2021. Ambapo Mhe. Rais Samia amekamilisha ziara yake ya siku mbili Nchini Burundi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye wakishuhudia utiaji saini hati ya makubaliano kuhusu baadhi ya mamb

UWEKAJI JIWE LA MSINGI KATIKA SKULI YA MTONI KIDATU ZANZIBAR

Image
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, ameuhimiza uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kuzingatia maslahi na thamani ya walimu katika utekelezaji wa majukumu yao kwa lengo la kukuza ubora katika sekta ya elimu nchini. Mheshimiwa Othman ameyasema hayo katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa banda la kusomea katika Skuli ya Mtoni Kidatu, Wilaya ya Magharibi 'A' Unguja. "Tutakapowawekea mazingira bora ya kazi, heshima, mishahara mizuri pamoja na kuthaminiwa katika kupata huduma za kijamii, tutawafanya walimu wetu kuwa na hamasa na kuukuza utendaji wao,”alieleza Makamu wa Kwanza wa Rais. Mheshimiwa Othman amesema walimu wamekuwa wakipata changamoto mbali mbali katika utekelezaji wa kazi zao, hivyo kuwajengea mazingira wezeshi ya kielimu na hata katika upatikanaji wa huduma za kijamii kutawapa uwezo wa kufanya kazi zao kwa ufanisi. "Hapo zamani mtu aliyekuwa na heshima kubwa katika kijiji ni mwalimu. H

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAPILI JULAI 18, 2021

Image