Posts

MHE.GEKUL: KUMBI ZA BURUDANI TOENI FURSA KWA BENDI ZA MUZIKI WA DANSI NA WASANII WACHANGA

Image
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul ametoa wito kwa wawekezaji wa kumbi za burudani nchini kutoa fursa kwa bendi za muziki wa dansi na wasanii wachanga kufanya maonesho  katika kumbi hizo ili kukuza na kuendeleza  Sanaa  nchini. Mhe. Gekul amesema hayo Juni 25, 2021 mjini Kahama wakati akifungua eneo la kisasa la burudani lenye hadhi ya Kimataifa la "The Magic 101". "Natoa rai kwa wasimamizi wa eneo hili kutoa fursa kwa bendi za muziki wa dansi hususani bendi kongwe pamoja na wasanii wachanga wa hapa Shinyanga na maeneo mengine ya nchi kufanya maonesho katika eneo hili ili waweze kuonesha vipaji vyao na kujiongezea kipato" amesema Mhe. Gekul. Mhe.Gekul amesema pamoja na kutoa fursa kwa vijana kutumia ukumbi huo pia amewaasa kutunza na kulinda maadili ya Mtanzania pamoja na kuwalinda vijana wadogo,  amesema hategemei kuwakuta wanafunzi na watoto wenye umri chini ya miaka 18 katika eneo hilo. Aidha, Naibu Waziri amewapongeza wamiliki

MAVUNDE: CHAGAMKIENI MIKOPO YA NYUMBA, VIWANJA

Image
Na Mwandishi Wetu, Dodoma MBUNGE wa Dodoma Mjini, Mhe. Anthony Mavunde amewahamasisha watumishi wa Kituo cha afya Makole kuchangamkia fursa ya kununua nyumba na viwanja vya makazi, katika mpango unaoendeshwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Benki ya Azania. Mhe. Mavunde alisema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dodoma alipokuwa akipokea vifaa tiba vilivyotolewa na PSSSF kwa Kituo cha afya Makole kama sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa umma iliyoadhimishwa kuanzia Juni 16 hadi 23, 2021. “Ndugu wafanyakazi wa kituo cha Makole, nawahamasisha jitokezeni kutumia fursa hii ya kumiliki nyumba na viwanja kama walivyosema wenzetu wa PSSSF, kwa mpango huu wa kulipa kidogo kidogo, naamini kila anaweza kupata anachotaka, hivyo jitokezeni” alisisitiza Mhe. Mavunde. PSSSF kwa kushirikiana na Benki ya Azania wana utaratibu wa kukopesha nyumba zilizojengwa na Mfuko na viwanja kwa Wanachama wake na Wananchi kwa ujumla kwa riba nafuu na masharti rafik

TAALUMA YA FAMASI NI MUHIMU KATIKA VITA YA NCD: Dkt. GWAJIMA

Image
 Na Catherine Sungura-WAMJW-Mwanza Katika vita dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza Taaluma ya Famasi ni muhimu katika kuwezesha upatikananji wa bidhaa  za dawa  kwa wale watakaoshindwa  kuzuia kupata  magonjwa yasiayoambukiza na ikawalazimu wafike vituoni  kupata tiba. Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima wakati wa Kongamano la 12 la kisayansi la Chama cha Wanafunzi wa Taaluma ya Famasi (TAPSA) lililofanyika jijini Mwanza. Dkt. Gwajima amebainisha kwamba bidhaa hizo za dawa kwa ajili ya kundi hilo  ni ghali na bahati mbaya  nchini Tanzania hakuna  kiwanda cha kutengeneza  na badala  yake wanaagiza toka nje ya nchi.“Tunapaswa kutafakari iwapo kasi ya kukua kwa maradhi haya ni inaongezeka je tunazijazititi vipi kwenye kasi ya kinga kwani bado kasi hiyo ni ndogo”.Aliongeza Dkt. Gwajima. Alisema kuwa, katika kupambana na magonjwa yasiyoambukiza Serikali  imeendelea kuboresha upatikanaji wa huduma bora  karibu zaidi na wan

NAIBU WAZIRI AFANYA ZIARA GEREZA ISANGA JIJINI DODOMA ASIKILIZA MAONI MBALIMBALI YA WAFUNGWA NA MAHABUSU

Image
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo (wanne kushoto), akiangalia moja ya bidhaa inayotengenezwa na wafungwa wanawake wa Gereza Isanga,baada ya kumaliza kikao cha kusikiliza maoni mbalimbali ya wafungwa hao.Ziara hiyo imefanyika Juni 27, 2021 jijini Dodoma. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo(wapili kushoto), akiangalia moja ya bidhaa inayotengenezwa na wafungwa wanawake wa Gereza Isanga,baada ya kumaliza kikao cha kusikiliza maoni mbalimbali ya wafungwa hao.Ziara hiyo imefanyika Juni 27, 2021 jijini Dodoma. Mkuu wa Gereza Isanga, Mrakibu wa Magereza Chausiku Kizigo akimkabidhi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo moja ya bidhaa inayotengenezwa na wafungwa wanawake katika gereza hilo baada ya kumaliza kikao cha kusikiliza maoni mbalimbali ya wafungwa hao.Ziara hiyo imefanyika Juni 27, 2021 jijini Dodoma. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo (watatu kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi w

KATIBU MTENDAJI AfCFTA AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI

Image
Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) Mhe. Wamkele Mene akipokelewa na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz. Kushoto mwa Mhe. Mene ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Biashara,Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji, kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Benard Haule. Mkurugenzi wa Idara ya Afrika – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz akiteta jambo na Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) Mhe. Wamkele Mene mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) Mhe. Wamkele Mene akipokelewa Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) Mhe. Wamkele Mene akipokelewa akipokelewa na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Us

RC TABORA AWAHIMIZI WAFANYABIASHARA MNADANI IPULI KUCHUKUA TAHADHARI YA KUJIKINGA NA COVID 19

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (Mwenye barakoa)akipata maelezo kutoka kwa mfanyabiashara wa ng'ombe wakati wa ziara yake kukagua ukusanyaji wa mapato na tahadahri zinachukuliwa dhidi ya virusi vya Corona katika Mnada wa Ipuli, mkoani humo Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (wa tatu kutoka kushoto)akipata maelezo kutoka Daktari wa Mifugo Mkoa wa Tabora . Dkt. Robert Machibya wakati wa ziara yake jana ya kukagua ukusanyaji wa mapato na kuangalia tahadhari zinachukuliwa dhidi ya virusi vya Corona katika Mnada wa Ipuli. Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (wa tatu kutoka kushoto)akiangalia ng’ombe wa mbegu kutoka Biharamulo ambazo zilikuwa zikiuzwa wakati wa ziara yake kukagua ukusanyaji wa mapato na kuangalia tahadhari zinachukuliwa dhidi ya virusi vya Corona katika Mnada wa Ipuli. Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (wa tatu kutoka kushoto)akipata maelezo kutoka Muuzaji wa Ng’ombe wa Mbegu kutoka Biharamulo , Bw. Har

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMATATU JUNI 28, 2021

Image