TANZANIA YAPATA MKOPO WA DOLA MILIONI 140 KUTOKA AfDB KUTEKELEZA MRADI WA UMEME MTO MALAGARASI, KIGOMA
Na, Saidina Msangi na Ramadhani Kissimba, WFM, Dar es Salaam Serikali ya Tanzania na Benki ya Maendeleo ya Afrika zimesaini mikataba miwili ya mkopo wenye thamani ya dola za Marekani milioni 140 (takriban shilingi bilioni 323.4) kwa ajili ya kufadhili Mradi wa kufua Umeme wa nguvu ya maji - Malagarasi. M i kataba y a mkopo huo wenye masharti nafuu imesainiwa Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba, kwa niaba ya Serikali na Bi. Nnenna Nwabufo, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Kanda ya Afrika Mashariki . Akizungumza wakati wa kusainiwa kwa M i kataba hiyo, Bw. Tutuba alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo utaijengea TANESCO uwezo wa usambazaji wa vifaa vya kuunganisha wateja 4,250 katika Wilaya za Kigoma, Kibondo na Kasulu ikiwemo kaya 1,000 zenye kipato cha chini, zahanati 4 na shule za msingi 6. “Mradi huu utahusisha ujenzi wa kituo kipya cha uzalishaji wa umeme wa gridi ya 49.5 MW chenye uwezo wa kuzalis