Posts

RAIS WA ZANZIBAR DKT. HUSSEIN ALI MWINYI AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UFARANSA NCHINI TANZANIA IKULU

Image
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiania na Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania Mhe.Frederic Clavier kwa kugonganisha mikoni alipowasili katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha leo 27-4-2021.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania Mhe. Frederic Clavier (kulia kwa Rais) akiwa na ujumbe wake, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha, mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.leo 27-4-2021.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania Mhe. Frederic Clavier, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha, mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbiu wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hus

HUDUMA YA MAMA NA MTOTO YATAKIWA KUWEPO KATIKA NGAZI ZOTE ZA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA NCHINI

Image
  Na.Catherine Sungura,WAMJW-Morogoro Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima ameagiza majengo yote ya vituo vya kutolea Huduma ambayo bado hayajaanza kutoa Huduma za afya kote nchini kuanza Mara moja kutoa Huduma za mama na mtoto ikiwemo utoaji wa chanjo ili kupunguza changamoto za afya. Dkt. Gwajima ameyasema hayo leo mkoni Morogoro wakati akifungua maadhimisho ya wiki ya chanjo ambayo Kitaifa yamefanyika Kwenye viwanja vya Chamwino. Dkt. Gwajima amesema kuwa yapo majengo mengi yamejengwa lakini hayajaanza kutoa huduma za Magonjwa ya nje (OPD) na kuagiza yaanze Sasa kutoa huduma za mama na mtoto ikiwemo Chanjo ili kuwapunguzia mwendo mrefu akina mama wajawazito na Watoto. Kwa upande wa maadhimisho ya wiki ya Chanjo Dkt. Gwajima amesema madhumuni ya wiki hii ni kuhamasisha na kuelimisha Jamii kuhusu umuhimu wa huduma za Chanjo Katika kukinga Magonjwa yanayozuilika kwa Chanjo na kuepusha vifo vinavyoweza kuzuilika kwa Chanjo. "Ninawahimiza

WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA KUUNGANISHA MAGARI CHA BM MOTORS NA KIWANDA CHA MADAWA KAIRUKI, KIBAHA MKOANI PWANI

Image
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua basi, lililounganishwa na kiwanda cha kuunganisha mabasi cha BM Motors, kilichopo Zegereni Kibaha mkoani Pwani, kinachomilikiwa na Mtanzania Bw. Jonas Nyagawa Aprili 27, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiingia kwenye basi, lililounganishwa na kiwanda cha kuunganisha mabasi cha BM Motors, kilichopo Zegereni Kibaha mkoani Pwani, kinachomilikiwa na Mtanzania Bw. Jonas Nyagawa Aprili 27, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Madawa cha Kairuki, Dk. Muganyizi Kairuki (kushoto), wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Zegereni Kibaha mkoani Pwani, Aprili 27, 2021. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Meneja wa Kiwanda cha Madawa cha Kairuki, Ellen Magita, wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Zegereni Kibaha mkoani Pwani, Aprili 2

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMATANO APRILI 28, 2021

Image
 

MALARIA YAENDELEA KUWASAKAMA WATOTO MKOANI SINGIDA

Image
Afisa Afya katika Kituo cha Afya Sokoine mjini Singida, Malangwa Joseph Seni akimpima uzito mmoja wa watoto waliohudhuria Kliniki hiyo. Bango lililobeba Kaulimbiu ya Siku ya Malaria Duniani mwaka huu likiwa mbele ya moja ya majengo ya Kituo cha Afya Sokoine mjini Singida. Baadhi ya wateja wakisubiri kupata huduma ya  mama  baba na mtoto Kituo cha Afya Sokoine mjini Singida.  Na Abby Nkungu, Singida  IMEBAINIKA kuwa malaria bado ni tatizo kubwa linalosumbua watoto mkoani Singida kutokana na takwimu za idara ya afya kuonesha kuwa zaidi ya asilimia 30 ya wanaougua ugonjwa huo na kwenda kupatiwa matibabu kwenye vituo vya huduma wana umri chini ya miaka mitano. Hayo yalibaika juzi Aprili 25 mwaka huu Tanzania ilipoungana na Nchi nyingine Wanachama wa  Shirika la  Afya Duniani (WHO)  kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani chini ya kauli mbiu “Ziro Malaria inaanza na mimi–Nachukua hatua kuitokomeza”   Taarifa ya idara ya afya  iliyotolewa na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa  wa Singida, Dk Ernest Muget

NAIBU WAZIRI KIGAHE:KUSAIDIA KUTATUA CHANGAMOTO ZA KIWANDA CHA PARETO MUFINDI

Image
  Naibu waziri wa viwanda na biashara Exaud kigahe akiwaeleza jambo viongozi wa kiwanda cha Pareto kilichopo wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa alipofanya ziara ya kusaidia kutatua changamoto za kiwanda hicho Na Fredy Mgunda,Mufindi. Naibu waziri wa viwanda na biashara Exaud kigahe amewahakikishia wamiliki wa kiwanda cha pareto kilichopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kuwa atawasaidia kutatua changamoto wanazokabiliwa nazo katika uendesheji wa kiwanda hicho ambacho kimekuwa manufaa makubwa kwa wananchi wa wilaya hiyo na taifa kwa ujumla. Akizungumza mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea kiwanda hicho naibu waziri Kigahe   alisema kuwa amebaini kuwa kiwanda hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali kama kuwepo kwa biashara ya zao hilo kimagendo na kusababisha wakulima kunyonywa na walanguzi hao.   Alisema kuwa walanguzi hao wamekuwa wananua zao la pareto kwa bei ndogo huku wakitumia mizani ambayo inawanyonya wakulima hivyo amepiga marufuku kwa walangiuzi hao kuacha mara moj

NAIBU WAZIRI WA ARDHI AWAONYA WANAOTUMIA VIONGOZI KUKWEPA KULIPA KODI SINGIDA

Image
  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabula akiongea na wadaiwa sugu na kutoa ufafanuzi wa msamaha wa kodi kwa taasisi za dini. Baadhi ya wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi wakimsikiliza Mh.Dkt. Angeline Mabula, Naibu Waziri wa Ardhi alipofika mkoani Singida kuzungumza nao. Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabula akipata maelezo kuhusu nyumba zinazopangishwa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabula akiza katika picha ya pamoja na watumishi wa ofisi ya Ardhi ya Mkoa ya Singida mara baada ya kumaliza Ziara yake mkoani humo.   Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Angeline Mabula amefanya ziara ya siku moja Mkoani Singida kwa lengo la kukukutana na wadaiwa wenye madeni ya muda mrefu (wadaiwa sugu), kujadili changamoto zao na kutafuta suluhisho kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria dhidi yao. Naibu Waziri Mabula amechukua h