Posts

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAMOSI MACHI 27, 2021

Image
 

RAIS SAMIA AONGOZA MAELFU MAZISHI YA JPM

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiweka udongo wakati wa mazishi ya Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwenye makaburi ya familia nyumbani kwake Chato mkoani Geita Machi 26, 2021. Rais ameongoza maelfu ya WATU kutoka kada mbalimbali nchini KATIKA mazishi hayo.  

KUTOKA MAGAZETINI LEO IJUMAA MACHI 26, 2021

Image
 

VIONGOZI, WASANII NA MAELFU YA WANANCHI WATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA HAYATI DKT MAGUFULI KIJIJINI CHATO MKOANI GEITA LEO

Image
Joseph, mtoto wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Joseph, mtoto wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitoa heshima zake za mwisho katika Uwanja  wa Magufuli kijijini Chato mkoani Geita leo Machi 25, 20121 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdullah akiongoza wananchi kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Uwanja wa Magufuli kijijini Chato mkoani Geita leo  Machi 25, 20121 Sehemu ya ndugu wa karibu wa marehemu wa aliyekuwa Rais wa  Jamhuriya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Uwanja  wa Magufuli kijijini Chato mkoani Geita leo Machi 25, 20121(PICHA  NA IKULU). Viongozi mbalimbali wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa  aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  katika Uwanja wa Magufuli kijijini Chato mkoani Geita  leoMachi 25, 2012

CHATO WABUBUJIKWA NA MACHOZI

Image
SHUGHULI ya kuaga mwili wa marehemu Dkt. John Pombe Magufuli imeacha simanzi huku Wakazi wa Chato na maeneo jirani wakibubujikwa na machozi wakati wa kuaga mwili wa Kiongozi huyo aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uwanja wa Magufuli wilayani humo leo Machi 25, 2021. Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ndiye aliyeongoza shughuli hiyo itakayofuatiwa na mazishi yatakayofanyika Ijumaa Machi 26, 2021.