Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) akizungumza na wasimamizi wa mradi wa Kiwanda cha Machinjio ya Kisasa cha Nguru Hills pamoja na Viongozi wa Mkoa na Ranchi hiyo ya Nguru Hills alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo Mvomero, Mkoani Morogoro. Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo. Na. Mwandishi Wetu – Morogoro Imeelezwa kuwa Sekta ya Hifadhi ya Jamii ikitumika vizuri itawezesha kukuza kasi maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi na taifa kwa ujumla endapo itawekeza kwenye maeneo au miradi ya kimkakati. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama wakati akitoa majumuisho ya ziara yake alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa Kiwanda cha Machinjio ya Kisasa cha Nguru Hills kilichopo Mvomero, Mkoani Morogoro. Akik