WAJUMBE WA BODI YA MKURABITA WATEMBELEA KITUO JUMUISHI CHA BIASHARA NJOMBE
KAMATI ya Uongozi ya Mpango wa Urasimishaji Ardhi na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Balozi mstaafu Daniel Ole Njoolay imetembelea Kituo Jumuishi cha Biashara kilichopo Halmashauri ya Mji wa Njombe. Walipofika katika kituo hicho walielezwa na Afisa Biashara wa Halmashauri, George Mwaseba kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa katika kituo hicho ambacho kimewezeshwa na Mkurabita samani na vitendea kazi vikiwemo kompyuta 3, scanner, Printer na meza ambavyo vimerahisisha kazi na kuifanya halmashauri kuongeza mapato kupitia malipo ya leseni za biashara. Mwaseba amesema uwepo wa kituo hicho umewapunguzia usumbufu wananchi kwani sasa huduma karibu zote zinapatikana hapo. Mwenyekiti wa Bodi ya Mpango wa Urasimishaji wa Ardhi na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), Balozi mstaafu Daniel Ole Njoolay (kushoto) pamoja na wajumbe wa bodi hiyo, wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Biashara wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, George Mwaseba kuhusu Kitu