Posts

RAIS MHE. DKT. MAFUFULI AZINDUA MRADI WA MAJI ISAKA-KAGONGWA MKOANI SHINYANGA

Image
 

FEDHA ZACHELEWESHA NHC KUKAMILISHA MRADI HOSPITALI YA RUFAA MARA

Image
  FEDHA ZACHELEWESHA NHC KUKAMILISHA MRADI HOSPITALI YA RUFAA MARA    Na  Munir Shemweta, WANMM MUSOMA   Imebainika kuwa kuchelewa kupelekwa fedha katika mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara iliyopo eneo la Kwangwa kumesababisha Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kutokamilisha mradi huo kwa wakati.   Mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara ulianza kujengwa  na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Septemba 15, 2019 na kutarajiwa kukamilika Agosti 2020 ambapo hata hivyo Mkandarasi (NHC) aliomba kuongezewa muda wa miezi sita (6) kutokana na kazi zilizoongezeka nje ya mkataba pamoja na kuchelewa kupatikana Wakandarasi maalum wa mradi.   Akiwa katika ziara ya siku moja katika mkoa wa Mara tarehe 28 Januari 2021 kukagua utendaji wa sekta ya ardhi na kuhamasisha ukusanyaji kodi ya Pango la ardhi, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula  alielezwa na Katibu Tawala wa mkoa Mara Catherine Mthapura akiwa kwenye ofisi ya Mkuu wa mkoa kuwa, a

SERIKALI: TUNACHUKUA HATUA MADHUBUTI KULINDA NGUVUKAZI YA NCHI

Image
  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu, Ummy Nderianaga, akiwahutubia washiriki wa mafunzo ya Huduma ya Kwanza ambao ni watumishi wa TANESCO alipohitimisha mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Mwanza. Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu, Ummy Nderianaga, akikabidhi vyeti kwa washiriki wa mafunzo ya Huduma ya Kwanza ambao ni watumishi wa TANESCO alipohitimisha mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Mwanza. Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, akitoa maelezo ya awali mbele ya Mgeni Rasmi (Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu) wakati wa kufunga mafunzo ya Huduma ya Kwanza yaliyotolewa na OSHA kwa watumishi wa TANESCO. Mkufunzi kutoka OSHA, Nathanael Mbwambo, akifundisha somo la Huduma ya Kwanza kwa vitendo katika mafunzo hayo yaliyotolewa kwa watumishi wa TANESCO jijini Mwanza. ******************************************** Na Mwandishi Wetu Serikali imes

MOI YAWEKA HISTORIA KWA MARA YA KWANZA IMEANZA KUTOA HUDUMA YA UCHUNGUZI WA MISHIPA YA DAMU KWENYE UBONGO BILA KUFUNGUA FUVU

Image
  Mgonjwa akifanyiwa uchunguzi wa mishipa ya damu kwenye ubongo bila ya kufungua fuvu katika maabara ya kisasa ya upasuaji wa Ubongo (Angio Suite ) iliyopo MOI. Huyu ni mgonjwa wa kwanza toka ujenzi wa maabara hiyo yenye thamani ya Tsh Bilion 7.9 ikamilike. Madakati bingwa wakifanya huduma ya uchunguzi wamishipa ya damu kwenye ubongo bila kufungua fuvu. Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akiwa na Mkurugenzi wa tiba MOI Dkt Samuel Swai pamoja na madaktari wengine wakifuatilia huduma ya uchunguzi wa mishipa ya damu kwenye ubongo bila kufungua fuvu wakiwa katika chumba maalum ambacho waliweza kushuhudia upasuaji moja kwa moja. Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akiwa katika picha ya pamoja na jopo la madaktari bingwa, wauguzi na wataalamu wa radiolojia kutoka MOI, MNH, AGHAKHAN na JKCI walioshiriki katika tukio la kihistoria la kuchunguza ubongo bila kufungua fuvu. ******************************************* Taasisi ya Mifupa Muhimbili- MOI Imeandi

WAZIRI KALEMANI ATOA MIEZI 6 KWA MKANDARASI WA KITUO CHA KUPOZA UMEME LUGURUNI KUKAMILISHA UJENZI

Image
 WAZIRI KALEMANI ATOA MIEZI 6 KWA MKANDARASI WA KITUO CHA KUPOZA UMEME LUGURUNI KUKAMILISHA UJENZI Na Dorina Makaya - Dar-es-salaam Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani ametoa miezi 6 kwa Mkandarasi anayejenga kituo kipya cha Kupoza umeme Luguruni kukamilisha ujenzi wa kituo hicho. Waziri Kalemani ametoa agizo hilo tarehe 28 Januari, 2021 alipofanya ziara kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho jijini Dar-e-salaam. Waziri Kalemani amebainisha kuwa, Mradi mzima wa kujenga kituo hiki cha kupoza umeme Luguruni utagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 15.2 na kuwa fedha hizo zimetolewa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 100. Waziri Kalemani amefafanua kuwa, ameamua kutembelea kituo hicho ili kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho kutokana na umuhimu wake hasa kitakapokamilika. Waziri Kalemani amesema, hapa nchini tunajenga vituo vingi sana vya kufua umeme ama kupoza umeme. “tumeshajenga vituo zaidi ya 134 mpaka sasa na tumekamilisha vituo vipya 24 hivi karibuni vikiwemo vya S

TMDA INADHIBITI UTENGENEZAJI NA UINGIZAJI WA DAWA NA VIFAA TIBA KUHAKIKISHA USALAMA KWA WATUMIAJI

Image
  Meneja wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA Kanda ya Ziwa Sophia Mziray akielezea kuhusu wanavyodhibiti Dawa na Vifaa tiba vinapotengenezwa au kuingizwa nchini na kwenye masoko Ofisi ya Mamlaka ya Dwa na Vifaa Tiba Kanda ya Ziwa. ......................................................... Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Ziwa imesema inafanya kazi ya kudhibiti wa Dawa na Vifaa Tiba ikiwa ni kuhakikisha wananchi wanapata Dawa na Vifaa vyenye ubora,Usalama na Ufanisi. Imesema kuwa imekuwa na ufatiliaji dawa katika mnyororo mzima wakati inaingia na wakati usambazi kutoka chanzo Kikuu na kwenda kwa watumiaji. Hata hivyo amesema wafanyabiasha wafuate taratibu kwani hawawezi kupitisha dawa na ikaendelea kuumiza wananchi wamejipanga kila sehemu ya mipaka ili khakikishakila kitu kinakwenda sawa. Akizungumza na waandishi wa Habari katika Ofisi za Kanda ya Ziwa hivi karbuni Meneja  Meneja wa TMDA Sofia Mziray Kanda hiyo amesema kuwa udhibiti wa Dawa na Vifaa Tiba unahitaji

KUTOKA MAGAZETINI LEO IJUMAA JANUARI 29, 2021

Image
 

FURAHA BAADA YA RAIS MAGUFULI KUMSAMEHE MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA KAHAMA BW. ANDERSON MSUMBA KWA KUNUNUA GARI LA GHARAMA KUBWA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mawaziri, pamoja na viongozi wengine wa mkoa wa Shinyanga akiweka jiwe la msingi ujenzi wa Kiwanda cha Nafaka, Vinywaji na Maziwa (Kom Limited) Kahama mkoani Shinyanga leo tarehe 28 Januari 2021. Kiwanda hicho kinatarajiwa kuanza kufanya kazi Mwezi Julai mwaka huu. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telak ili aweze kumsaidia Mama Cristina Masigwa ambaye anadai kudhulumiwa kipande cha Ardhi mkoani Shinyanga. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Chapulwa Kahama mara baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Kiwanda cha Nafaka, Vinywaji na Maziwa (Kom Limited) Kahama mkoani Shinyanga leo tarehe 28 Januari 2021.  Baadhi ya viongozi mbalimbali pamoja na wabunge wakipiga makofi mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk

NAIBU WAZIRI UMMY ATEMBELEA MIRADI YA KIUCHUMI YA WATU WENYE ULEMAVU

Image
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga (wa pili kutoka kulia) akimsikiliza Bw. Emmanuel Mussa Kashinje (kushoto) Mjasiriamali mwenye ulemavu ambaye amenufaika na mkopo wa asilimia 2 unaotolewa na Halmashauri kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt. Phillis Meshack, (wa pili kutoka kushoto) ni Kaimu Mkurugenzi wa Watu wenye Ulemavu Bw. Jacob Mwinula. Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga (kulia) akizungumza na Bw. Emmanuel Mussa Kashinje (kushoto) Mjasiriamali mwenye ulemavu anayejishughulisha na Uwakala wa huduma za kifedha alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya kiuchumi ya Watu wenye ulemavu Jijini Mwanza. (Katikati) ni Kaimu Mkurugenzi wa Watu wenye Ulemavu Bw. Jacob Mwinula. Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga akiangal