Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Geogre Simbachawane akiagana na mmoja wa Makandarasi wanaojenga Reli ya Mwendokasi (SGR) baada ya barabara inayoenda Kijiji cha Pwaga kujaa maji na magari kushindwa kupita katika eneo la Gulwe, Wilayani Mpwapwa, Mkoani Dodoma, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Na Mwandishi Wetu, MOHA, Pwaga. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Geogre Simbachawane amewataka Watanzania kutunza amani iliyopo nchini na pia kuenzi misingi ya maadili mema yaliyoachwa na Waasisi wa Taifa. Amesema amani na upendo uanzia katika familia, hivyo katika kipindi cha sikukuu ya Krismasi familia zinajenga upendo na amani, hivyo amani hiyo iwe pia katika kujenga Taifa. Simbachawene amezungumza hayo katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria wa Rozali Pwaga, Jimbo la Kibakwe, Wilayani Mpwapwa, leo, ambapo mamia ya waumini walihudhuria misa hiyo, ambayo pia iliombwa na familia ya Marehemu Mzee Simbachawene wakiwaombea marehemu mbalimbali wa ukoo huo. “Familia ziishi k