Posts

NAIBU WAZIRI CHILO ATEMBELEA IDARA YA UHAMIAJI MKOA WA KUSINI PEMBA

Image
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Khamis Hamza Chilo,akizungumza na viongozi wa juu wa Idara ya Uhamiaji mkoa wa Kusini Pemba leo, wakati wa ziara ya kikazi.Watatu kushoto ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar,Johari Sururu. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo,akikaribishwa dafu baada ya kumaliza ziara ya kikazi katika Ofisi ya Idara ya Uhamiaji,Mkoa wa Kusini Pemba Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Khamis Hamza Chilo,akiongozana na Askari wa Uhamiaji leo, wakati wa ziara ya ukaguzi wa nyumba za askari wa uhamiaji (zinazoonekana pichani), zilizopo Wilaya ya Ckakechake, mkoa wa Kusini Pemba.

WAZIRI LUKUVI AANZA KUWASAKA WAMILIKI WA ARDHI WASIOCHUKUA HATI KWA SIMU

Image
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiwa katika zoezi la kuwapigia simu  wamiliki wa ardhi katika jiji la Dar es Salaam walioshindwa kuzifuata hati zao zilizokamilika kwenye ofisi za ardhi za mikoa. Kushoto ni Msajili wa Hati Msaidizi mkoa wa Dar es Salaam Juma Ligela. Jumla ya Hati 20,752 hazijachukuliwa na wamiliki wake katika ofisi za ardhi za mikoa. Na Munir Shemweta, DAR ES SALAAM Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ameanza kazi ya kuwatafuta wamiliki wa ardhi walioshindwa kuchukua hati zao kwenye ofisi za Ardhi za mikoa kwa kuwapigia simu wamiliki wa jiji la Dar es Salaam na  kuwataka kuzifuata hati zao katika kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Desemba 29, 2020. Jumla ya Hati 20,752 hazijachukuliwa katika ofisi za ardhi kwenye mikoa 26  ya Tanzania Bara na hivyo kufanya kuwepo mlundikano wa hati katika ofisi za Wasajili wa Hati Wasaidizi katika Ofisi za Ardhi za mikoa. Miongoni mwa wamiliki wa ardhi waliopigiwa simu ni kutoka maeneo

DKT. NDUGULILE AHIMIZA TAASISI ZA SERIKALI KUHIFADHI DATA ZAO

Image
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wa Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Data (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kutembelea taasisi hiyo, Dar es Salaam. Anayesikiliza ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula  Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo A. Mathew akizungumza na wafanyakazi wa Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Data (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani) ya kutembelea taasisi hiyo, Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa taasisi hiyo, Geofrey Mpangala. Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula akizungumza na wafanyakazi wa Kituo cha Kuhifadhi Data (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Waziri wa Wizara hiyo, Dkt.Faustine Ndugulile (wa kwanza kushoto) ya kutembelea taasisi hiyo. Wa nne kulia nia Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzan Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya H

WAZIRI SIMBACHAWENE AWATAKA WATANZANIA KUTUNZA AMANI, ASEMA NCHI IPO SALAMA, MADEREVA WAACHE MIHEMKO BARABARANI MWAKA MPYA

Image
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Geogre Simbachawane  akiagana na mmoja wa Makandarasi wanaojenga Reli ya Mwendokasi (SGR) baada ya barabara inayoenda Kijiji cha Pwaga kujaa maji na magari kushindwa kupita katika eneo la Gulwe, Wilayani Mpwapwa, Mkoani Dodoma, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Na Mwandishi Wetu, MOHA, Pwaga. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Geogre Simbachawane amewataka Watanzania kutunza amani iliyopo nchini na pia kuenzi misingi ya maadili mema yaliyoachwa na Waasisi wa Taifa.  Amesema amani na upendo uanzia katika familia, hivyo katika kipindi cha sikukuu ya Krismasi familia zinajenga upendo na amani, hivyo amani hiyo iwe pia katika kujenga Taifa. Simbachawene amezungumza hayo katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria wa Rozali Pwaga, Jimbo la Kibakwe, Wilayani Mpwapwa, leo, ambapo mamia ya waumini walihudhuria misa hiyo, ambayo pia iliombwa na familia ya Marehemu Mzee Simbachawene wakiwaombea marehemu mbalimbali wa ukoo huo.   “Familia ziishi k

WANA VITUO VYA TAARIFA NA MAARIFA MSALALA WATINGA KISHAPU KUJINOA UANDAAJI BAJETI KWA MRENGO WA JINSIA

Image
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu, Emmanuel Johnson akizungumza wakati wa ziara ya Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa Halmashauri ya wilaya ya Msalala kwenye halmashauri ya Kishapu. Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala kata za Shilela na Lunguya wametembelea halmashauri ya wilaya ya Kishapu kwa ajili ya kujifunza kuhusu uandaaji wa bajeti ya mrengo wa kijinsia na umuhimu wake kupitia mradi wa Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wanawake kiuchumi unaotekelezwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kupitia shirika la Watu na Makazi Duniani (UNFPA). 

RAIS DKT MAGUFULI AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA DARAJA LA KIGONGO-BUSISI MKOANI MWANZA

Image
Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wananchi baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Darala la Kigongo-Busisi la urefu wa kilomita 3.2 mkoani Mwanza leo Jumatatu Desemba 28, 2020 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipungia wananchi wakati akiingia kwenye  kivuko baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Darala la Kigongo-Busisi la urefu wa kilomita 3.2 mkoani Mwanza leo Jumatatu Desemba 28, 2020 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipungia wananchi wakati akiingia kwenye  kivuko baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Darala la Kigongo-Busisi la urefu wa kilomita 3.2 mkoani Mwanza leo Jumatatu Desemba 28, 2020 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua maendeleo ya ujenzi wa Darala la Kigongo-Busisi la urefu wa kilomita 3.2 mkoani Mwanza leo Jumatatu Desemba 28, 2020

WAZIRI MKUU APOKEA VYUMBA 14 VYA MADARASA

Image
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea vyumba 11 vya madarasa, ofisi mbili za walimu, samani na chumba maalumu cha wasichana vilivyojengwa na Benki ya TPB PLC katika shule ya msingi Nandagala wilayani Ruangwa, Lindi kwa gharama ya shilingi milioni 164.902. Amepokea mradi huo wa ujenzi na ukarabati wa vyumba vya madarasa leo (Jumatatu, Desemba 28, 2020) alipotembelea shule hiyo akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani Ruangwa. Waziri Mkuu ameupongeza uongozi wa benki hiyo. Waziri Mkuu amewataka wazazi, walimu na wanafunzi wahakikishe majengo hayo yanatunzwa ili yaweze kutumika kwa muda mrefu. “Tunataka majengo haya kama yalivyo leo yaendelee kuwa hivihivi. Tuyatunze haya majengo, Wanafunzi msifanye majaribio ya kuandika ukutani wala kupiga chapa ya miguu kwenye ukuta. Tunawashukuru TBP kwa kutukabidhi madarasa haya ambayo manne ni mapya na saba yamekarabatiwa.” Akizungumzia kuhusu ufaulu, Waziri Mkuu amesema kati ya wanafunzi 63 waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu katika shul