Posts

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMANNE DESEMBA 29, 2020

Image
 

DKT. NDUGULILE AIPA TCRA MIEZI MITATU KUMALIZA CHANGAMOTO ZA VIFURUSHI NA BANDO KWA WANANCHI

Image
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Mhandisi James Kilaba (wa kwanza kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (wa tatu kulia) na Naibu Waziri wake, Mhandisi Kundo A. Mathew (wa pili kulia) kuhusu mifumo ya TEHAMA inayotengenezwa na taasisi hiyo. Wa nne kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo   Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo kwa Menejimenti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (hawapo pichani), wakati alipotembelea taasisi hiyo, Dar es Salaam. Na Prisca Ulomi, WMTH Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt.Faustine Ndugulile ameipa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) miezi mitatu kumaliza changamoto za bando na vifurushi zinazotolewa na kampuni za simu za mkononi kwa wananchi  Dkt. Ndugulile ameyasema hayo wakati wa ziara yake alipotembelea TCRA ikiwa ni moja ya taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kwa lengo la kufahamiana, kutambua majukumu yao na kuzun

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMATATU DESEMBA 28, 2020

Image
 

WAZIRI MKUU AMUAGIZA CAG AFANYE UKAGUZI MAALUMU TPA

Image
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwenda kufanya ukaguzi maalum katika bandari za Dar es Salaam, Mwanza, Mtwara, Tanga na Kyela kutokana na kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha za umma. Pia Waziri Mkuu amewasimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha wa TPA, Bibi Nuru Mhando pamoja na Meneja wa Matumizi ya Fedha wa TPA, Bibi Witness Mahela ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha zinazowakabili. Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo baada kupokea ripoti ya Ukaguzi Maalum uliofanywa na CAG katika hesabu ya Bandari ya Kigoma kwa mwaka 2017/2018 na 2018/2019. Lengo la ukaguzi huo lilikuwa kujiridhisha kuhusu matumizi mabaya ya fedha za umma. Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumapili, Desemba 27, 2020) katika kikao chake na Waziri na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Bodi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania na Menejimenti ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) ki

WAZIRI WA UTALII DKT. NDUMBARO AMPOKEA DREW AMBAYE ANA WAFUASI MILIONI 30 KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

Image
Mh Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas NDUMBARO akimpokea Drew Binsky, uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere, Dar es salaam, Tanzania tarehe 27 Disemba 2020. Bw Drew ambaye anawafuasi zaidi ya 30 milioni kwenye mitandao ya kijamii na mkewe Diana wanatembelea vivutio vya utalii Tanzania.  

MOTO WATEKETEZA MADUKA

Image
   Na Eliud  Rwechungura, Karagwe. Moto mkubwa umeunguza maduka zaidi ya 10 na kuteketeza baadhi ya vitu katika majengo yanayomilikiwa na familia ya Nekemia Kazimoto (Kazikomu)  yaliyopo Mji wa Kayanga mjini, Karagwe, mkoani Kagera. Maduka hayo yanayotazamana na majengo ya city center na Magereza ya Kayanga. Kwa mujibu wa mashuhuda moto huo umeibuka majira ya saa 5 na dakika 20 usiku  wa kuamkia leo katika moja ya duka la nguo na kusambaa katika maduka mengine ya bidhaa za vyakula, hoteli, stoo za vifaa vya ujenzi, saluni na maduka ya bidhaa mchanganyiko. Moto huo umedumu zaidi ya masaa manne na chanzo cha moto hakijafahamika mpaka sasa.  26 Disemba 2020.