Posts

WANAOFANYA MAPENZI NA WASICHANA WENYE UMRI MDOGO WAONYWA.

Image
Na WAMJW- Kilimanjaro  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ametoa onyo kali kwa wanaofanya mapenzi (ngono) na wasichana wenye umri mdogo, hali inayosababisha kuwaharibia malengo yao ya baadae.  Mhe. Kassim Majaliwa ameyasema hayo leo wakati akiwahutubia wananchi kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika katika uwanja wa Mandela Moshi, Mkoani Kilimanjaro yenye kauli mbiu ya "Mshikamano wa kimataifa, Tujumuike Pamoja". "Nataka niwakumbushe na kutoa tahadhari kwa wale watu wazima mnaofanya mapenzi na vija wadogo wa kike, ole wenu, ole wenu, ole wenu " ameyasema Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.  Alisema kuwa, takwimu za maambukizi mapya ya VVU zinaonesha kwamba asilimia 40 ya maambukizi hutokea kwa vijana na katika hao asilimia 80 ni vijana wa kike, huku akiweka wazi kuwa, vijana ni kundi linalokabiliwa na changamoto ya maambukizi mapya ya VVU nchini. Aliendelea kusema, kundi la vijana na hasa wa kike lipo kwenye h

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMATANO DESEMBA 2, 2020

Image
 

PEPPSI TANZANIA YAHIMIZA UPENDO KWA WATU WANAOISHI NA VVU

Image
  Mkurugenzi wa REPPSI  Edwick Mapalala  akiwa katika maonyesho ya siku ya ukimwi katika viwanja vya Posta, Kijitonyama Mkurugenzi wa REPPSI  Edwick Mapalala  akiwa na baadhi ya vijana katoka maonyesho ya siku ya ukimwi katika viwanja vya Posta, Kijitonyama Mwandishi wetu, Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkazi wa Shirika  Regional Psychosocial Support Initiative (REPPSI), Edwick Mapalala ameikumbusha jamii kuongeza upendo na kuendelea kutokomeza unyanyapaa kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU). Amesema kuwalinda, kuwathamini na kuwajali watu wanaoishi na VVU hasa vijana kutasaidia kuwapunguzia msongo wa mawazo wale ambao hawajaikubali afya yao, na hivyo kuikubali na kushiriki katika kukuza uchumi wa Taifa. Mapalala amesema hayo wakati akitoa salamu za REPPSI, Shirika linalojihusisha na malelezi, makuzi na msaada wa Kisaikolojia kwa watoto kuhusu siku ya Ukimwi Duniani. “Hii ni siku ya kutafakari kuhusu maambukizi ya VVU, waliopima na kujua afya zao waendelee kuwa waaminifu kwenye utu

Wanafunzi wapya 3,544 wapangiwa mikopo ya TZS 11.04 bilioni

Image
  Na Mwandishi Wetu,   BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha ya Awamu ya tatu yenye jumla ya wanafunzi wapya  3,544  waliopangiwa mikopo kwa mara ya kwanza katika mwaka wa masomo 2020/2021 yenye thamani ya  TZS 11.04 bilioni.   Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Jumanne Desemba Mosi, 2020 na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru ilisema ili kupata taarifa za kina kuhusu mikopo waliyopangiwa, wanafunzi hao  3,544  wanashauriwa kutembelea akaunti zao walizotumia kuomba mikopo kwa njia ya mtandao maarufu kama  SIPA – Student’s Individual Permanent Account (SIPA).   “Kufuatia kutolewa kwa awamu hii ya tatu, hadi sasa jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo ni  53,364  yenye thamani ya  TZS 173.29 bilioni . Aidha, jumla ya wanafunzi  69,625  wanaoendelea na masomo wamepangiwa  TZS 247.5   bilioni  baada ya kufaulu mitihani yao ya mwaka 2019/2020” alisema Badru.   Kufunguliwa kwa dirisha la rufaa   Badru alisema baada ya

WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI WASEMA ARV'S ZA SASA ZINAWAPENDEZESHA

Image
  Kijiji cha Jamii kilichopo katika uwanja wa shule ya msingi Mandela kata ya Pasua ambacho kimendaliwa na Baraza la Watu wanaoshi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA) kwa ajili ya kuendesha mijadala juu ya masuala ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi. Mwenyekiti wa Baraza la Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA) Leticia Maurice akizungumza wakati wa mjadala katika kijiji cha Jamii kilichowakutanisha viongozi wa dini mbalimbali nchini. Baadhi ya washiriki wa mjadla juu ya masuala mbalimbali ya Ukimwi wakifuatilia kwa karibu hoja zilizokuwa zikitolewa katika kijiji cha jamii. Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dkt Leonard Maboko akizungumza wakati wa mjadala katika kijiji cha jamii uliowashirikisha viongozi wa dini . Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la taifa la watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi (NACOPHA) Deogratius Rutatwa akizungumza wakati wa kongamano hilo. Askofu wa kanisa la Waadventista Wasabato jimbo la Bonde la Ufa ,Marco Barnabas akizungumza

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMANNE DESEMBA 1, 2020

Image