Posts

Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Habari Lajionea Ujenzi wa SGR

Image
Na Shamimu Nyaki -WHUSM, Morogoro.   Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi  wa  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  wa metembelea  M radi wa  K imkakati wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Morogoro - Dodoma ambapo wamefurahishwa na namna mradi huo unavyotekelezwa kwa kasi. Akizungumza kwa niaba ya baraza hilo ,  Novemba 27, 2020 Mkuu wa msafara ambaye  ni Mkurugenzi  wa  Idara ya Sera na Mipango, Bw. Petro Lyatuu ,  amesema kwamba ziara hiyo imekuwa na manufaa kwa kuwa wajumbe wa baraza wamejifunza kwa vitendo namna mradi unavyotekelezwa hatua kwa hatua. "Tumekua na siku nzuri leo tumejifunza kwa kuona jinsi Serikali inavyotekeleza mradi huu, tumeona hatua il i yofikiwa katika ujenzi ikiwemo usimikwaji wa nguzo za umeme pamoja na utandikaji wa mataruma ya reli, naamini tutakua mabalozi wazuri katika kuelimisha na kushawishi wengine waje wajifunze na kuona kazi inayofanyika hapa" amesema Bw. Lyatuu. Kwa upande wake Mhandisi Msaidizi wa Mradi kutoka Shirika la Reli Tanzan

TARURA YADHAMIRIA KUUNGANISHA WILAYA YA RUANGWA NA LIWALE

Image
N a Bebi Kapenya   Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), umeendelea kuboresha miundombinu ya barabara na madaraja katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi ikiwemo ujenzi wa daraja la Mto Mbwemkuru lenye urefu wa mita 75  linalojengwa katika barabara ya Chikwale hadi Liwale  kwa gharama ya Shilingi Bilioni 4.5. Meneja wa TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Mhandisi Mashaka Nalupi alisema mradi wa ujenzi wa daraja la Mto Mbwemkuru umetokana na mpango wa kuunganisha Wilaya ya Ruangwa na Wilaya ya Liwale kwa lengo la kurahisisha mawasiliano kwa wananchi wa maeneo hayo na kuwezesha shughuli zao za kiuchumi na kijamii kwa haraka. “ Wilaya hizi mbili ni maarufu sana katika kilimo cha korosho na ufuta, lakini pia wananchi wa vijiji vya Nangurugai, Mirui, Narungombe, Machang’anja na Chikwale watapata faida ya kiuchumi kwasababu mazao yao ya biashara yataweza kuvushwa kutoka upande wa Liwale kwenda Ruangwa ambapo kuna soko kubwa la mazao ya biashara pale Ruangwa mj

KAMATI YA USALAMA WILAYA YA IKUNGI SINGIDA YAKAGUA MIRADI YA ELIMU NA AFYA

Image
  Wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, wakijadiliana wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya Elimu na Afya wilayani humo. Kamati hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wake Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo. Moja ya chumba cha darasa kilicho kaguliwa na kamati hiyo. Baadhi ya madarasa yaliyokaguliwa. Muonekano wa vyoo vya Shule ya Msingi vilivyo kaguliwa na kamati hiyo. Muonekano wa baadhi ya madarasa yaliyokaguliwa na kamati hiyo. Muonekano wa baadhi ya madarasa yaliyokaguliwa na kamati hiyo. Ukaguzi ukiendelea.  Wajumbe wa kamati hiyo wakikagua ujenzi wa Chuo cha Veta. Kushoto mbele ni  Mwenyekiti wa kamati hiyo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo. Muonekano wa ndani wa baadhi ya madarasa ya shule za sekondari yaliyokaguliwa na kamati hiyo. Muonekano wa ndani wa baadhi ya madarasa ya shule za sekondari yaliyokaguliwa na kamati hiyo. Moja ya chumba cha darasa cha shule ya sekondari kilicho kaguliwa na kamati hiyo. Jengo la Maabara lililokaguliwa

MTATURU AANZA KUTEKELEZA AHADI ZA WANANCHI KWA KASI YA 4G

Image
  Wachungaji na waumini wa  Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)  Usharika wa Kiaskofu Msalaba Mrefu mjini Singida, wakiwa na pikipiki walizokabidhiwa hivi karibuni na Mbunge  wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu kwa ajili ya kazi za kanisa hilo, Mbunge  wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu, akimkabidhi pikipiki, Mkuu wa Jimbo la Kusini Usharika wa Issuna, Mchungaji, Obedi Msele. Mbunge  wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu, akimkabidhi pikipiki, Mchungaji Joyce Madadi wa Usharika wa Ikungi.   Mbunge  wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu, akimkabidhi pikipiki, Mchungaji, Felix Kibiriti. Na Dotto Mwaibale, Singida. MBUNGE wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu ameanza kutekeleza ahadi zake kwa wananchi kwa kasi ya 4G. Mtaturu ametekeleza ahadi yake  kwa kutoa pikipiki tano kwa Usharika wa Kiaskofu Msalaba Mrefu mjini Singida ambazo alimkabidhi Mchungaji Felix Kibiriti kwa niaba ya Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati Dkt. Alex Mkumbo kwa aj

SPIKA NDUGAI MGENI RASMI MAHAFALI YA CHUO CHA IFM JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai    akizungumza na Wahitimu wa Chuo cha    Chuo Kikuu cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wakati wa    Mahafali ya 46 chuo hicho yaliyofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam. Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai    (wa pili kushoto) akimpatia zawadi Mwanafunzi Bora kwa Wahitimu wa kozi zote za Shahada wa    Chuo cha Kikuu cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Bw. Robin Micky Goliama wakati wa    Mahafali ya 46 chuo hicho yaliyofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka    kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Tadeo Satta, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Prof. Emmanuel Mjema na Mwakilishi wa Waziri wa Fedha ambaye pia Naibu Mkurugenzi wa Mipango katika Wizara ya Fedha, Bw. David Mwankenja. Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai    (wa pili kushoto) akimpatia zawadi Mwanafunzi Bora kwa Wahitimu wa kozi zote za Shahada wa    Chuo cha Kikuu cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Bw. Robin Micky Goliama wakati wa    Mahafali ya 46 chuo hicho yaliyof

KATIBU MKUU KUSAYA AANZA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS MAGUFULI KUHUSU BIASHARA YA MAZAO YA KILIMO NJE YA NCHI

Image
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Kusaya leo mchana tarehe 27 Novemba, 2020 ameanza kutekeleza agizo la Rais, Dkt. John Pombe Magufuli la kuwataka Watendaji wa Wizara ya Kilimo kuendelea kujenga mazingira bora na wezeshi ya biashara ya mazao ya kilimo kwenda nje ya nchi kama alivyohutubia wakati wa kufungua Bunge la 12, tarehe 13 Novemba, 2020. Katika kulitekeleza agizo hilo Katibu Mkuu Kusaya amewatunuku vyeti Wakaguzi wa Ubora wa Mazao ya kilimo na Afya ya Mimea 32 kutoka Vituo vya ukaguzi vya mipakani na viwanja vya ndege vya Wizara ya Kilimo katika mikoa 18 ya Tanzania Bara. Katika hotuba yake hiyo; Rais John Pombe Magufuli alisema Serikali katika kipindi cha miaka hii mitano; Itanunua ndege ya kusafirisha mazao ya kilimo na itaboresha mazingira ya Sekta Binafsi kufanya biashara ya mazao ya kilimo kama mbogamboga, matunda, maua na viungo ambayo katika mwaka uliopita yaliingizia taifa fedha za kigeni kiasi cha dola milioni 779. Rais Magufuli aliongeza kuwa Serikali itanunua

TANZANIA YAIPONGEZA AfDB KWA KUENDELEA KUCHANGIA MIRADI YA MAENDELEO

Image
Na Farida Ramadhani na Ramadhani Kissimba – WFP Dar es Salaam Serikali ya Tanzania imeipongeza Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kuendeleza ushirikiano wao wa muda mrefu katika kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Pongenzi hizo zimetolewa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango wakati akimuaga aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini, Dkt. Alex Mubiru ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi katika ofisi ya Rais wa benki hiyo. Dkt. Mpango alisema kuwa benki hiyo imekuwa msaada mkubwa katika maendeleo ya nchi kutokana na mikopo mbalimbali ambayo imekuwa ikiitoa katika kutekeleza miradi ya kimkakati. “Dkt. Mubiru kupitia Benki ya Maendeleo ya Afrika amesaidia kusukuma fedha kwa ajili ya miradi ya kimkakati hapa nchini na katika miaka miwili aliyokaa hapa, Tanzania imeweza kunufaika na fedha za kutekeleza miradi yenye thamani ya takriban dola bilioni 2.5”, alisema Dkt. Mpango. Alisema miongoni mwa miradi

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAMOSI NOVEMBA 28, 2020

Image