MFUMO MPYA WA KITANZANIA WA TAARIFA ZA KIUTUMISHI NA MISHAHARA KUDHIBITI UINGIZWAJI WA TAARIFA ZISIZO SAHIHI
James Mwanamyoto, Dodoma Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala 108 waliohitimi Mafunzo ya siku 12 ya Mfumo Mpya wa Kitanzania wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara wametakiwa kukamilisha usahihishaji wa taarifa za watumishi zilizopo kwenye mfumo wa sasa ili ziweze kuingizwa katika mfumo mpya, kwani mfumo mpya hautoruhusu kuingiza taarifa ambazo sio sahihi na zisizokamilika. Maelekezo hayo yametolewa jana jijini Dodoma na Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Cosmas Ngangaji wakati akifunga mafunzo hayo yaliyokuwa na lengo la kuboresha utendaji kazi na usimamizi wa rasilimaliwatu na mishahara. Bw. Ngangaji amesema, baada ya kukamilika kwa mafunzo haya na kuanza kutumika rasmi kwa mfumo huu mpya, Serikali inatarajia mfumo mpya utatumika kutatua kero za watumishi kwa ufanisi na kwa haraka zaidi ikiwa ni pamoja na kuwaondolea usumbufu wa kufuata huduma Ofisi ya Rais Utumishi. Bw. Ngangaji ameongeza kuwa, mfumo mpya utaongeza uadilifu kiutendaji kwani umeweze