Posts

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAMOSI AGOSTI 29, 2020

Image
 

CCM KUZINDUA KAMPENI ZAKE LEO JIJINI DODOMA

Image
  Majukwa yakiendelea kupambwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma tayari kesho Agosti 29,2020 kwa mkutano wa  uzinduzi wa  kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli pamoja na Mgombea Mwenza,  Samia Suluhu Hassan. Uchaguzi Mkuu utafanyika Oktoba 28 mwaka huu. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA. Picha za Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli zikiwa zimepambwa kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma ambapo uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi Mkuu utafanyika kesho Jumamosi. Kijana muuza korosho Jamali Mohamed, akiangalia picha ya Mgombea Urais wa Tganzania kupitia CCM, Dk. Magufuli iliyopambwa kwenye Uwanja wa Jamhuri. Mambo yalivyo Uwanja wa Jamhuri Dodoma. Bendera za Chama Cha Mapinduzi zikiwa zimelipamba Jiji la Dodoma.  

VIDONDA VYA TUMBO VYAMFANYA WAZIRI MKUU JAPAN KUJIUZULU

Image
  NA K-VIS BLOG/MASHIRIKA YA HABARI WAZIRI Mkuu wa Japan Shinzo Abe amejiuzulu wadhifa huo leo Ijumaa Agosti 28,2020. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa, Bw. Abe mwenye umri wa miaka 65, amesema kujiuzulu kwake kunatokana na sababu za kiafya. Aidha imeelezwa kuwa Shinzo Abe ambaye ndiye Waziri Mkuu wa Japan aliyekaa kwenye nafasi hiyo kwa muda mrefu zaidi katika historia ya nchi hiyo amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya vidonda vya tumbo(ulcerative colitis) kwa muda mrefu. “Nisingependa maradhi Yangu yawe mjadala wa maamuzi kwa Wajapani,na ninaomba radhi kwa kushindwa kumaliza muhula wangu wa uongozi.”. alinukuliwa na vyombo vya habari akieleza katika taarifa take ya kujiuzulu

YANGA YAPATA KOCHA MPYA ZLATKO KRMPOTIC KUTOKA SERBIA

Image
  Klabu ya Yanga, imemtangaza Zlatko Krmpotic kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo, Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM, Injinia Hersi Said amesema hayo leo Asubuhi katika kipindi pendwa cha michezo cha Sports Arena leo asubuhi Agosti 28, 2020. Kocha huyo raia wa Serbia anatarajiwa  kuwasili nchini kesho Jumamosi, amesisitiza Injinia Hersi.

JAMBO YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MICHEZO KWA WANARIADHA MASHINDANO YA RIADHA KITAIFA 2020

Image
  Afisa Mauzo wa  Kampuni ya  Jambo Food Products Ltd, Alodia Ladislaus akimkabidhi jezi  Kaimu Afisa Michezo mkoa wa Shinyanga Talita Lupembe (wa pili kulia) kwa ajili ya  wanamichezo mkoa wa Shinyanga watakaoshiriki Mashindano ya Riadha Kitaifa yanayotarajiwa kufanyika Mwezi Septemba 2020 jijini Dar es salaam Na Kadama Malunde- Malunde 1 blog Kampuni ya Uzalishaji na Usambazaji Vinywaji Baridi Jambo Food Products Ltd imetoa msaada wa vifaa vya michezo na fedha kwa wanamichezo mkoa wa Shinyanga watakaoshiriki Mashindano ya Riadha Kitaifa yanayotarajiwa kufanyika Mwezi Septemba 2020 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es salaam. Akizungumza leo Alhamis Agosti 27,2020 Mwakilishi wa Wakurugenzi Kampuni ya Jambo Food Products Ltd, Halima Omary amesema Kampuni yao imetoa msaada wa vifaa vya michezo ili kuwapa ari na moyo wanariadha watatu kutoka mkoa wa Shinyanga  watakaoshiriki Mashindano ya Riadha Kitaifa mwaka 2020 . “Jambo Food Products Ltd ni wadau wakub

KAMISHNA CP LIBERATUS SABAS LEO AMEFAYA ZIARA YA KUKAGUA MPAKA WA TANZANZAIA NA ZAMBIA KATIKA MKOA WA SONGWE.

Image
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi CP Liberatus Sabas wa tatu kutoka kushoto akifuatiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe RPC George Kiando pamoja na maafisa wengine wa Jeshi la Polisi Mkoa   wa Songwe wakiwa Wilaya ya Momba wakikagua mpaka wa Tunduma (Tanzania) na Zimbia.  Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi CP Liberatus Sabas (katikati) Afisa kutoka TRA katika picha ya pamoja na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalamamkoa wa Songwe wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kikao kazi .(PICHA NA JESHI LA POLISI) Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi CP Liberatus Sabas, katikati akionyeshwa jiwe la Mpaka wa Tanzania na Zambia na   Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe RPC George kiando wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani huo leo 27/08/2020.

KUTOKA MAGAZETINI LEO IJUMAA AGOSTI 28, 2020

Image