Posts

SHIRIKA LA ESTL LATOA MAFUNZO KWA WAJUMBE WA KAMATI YA MTAKUWWA KATA YA MSANGE WILAYA YA SINGIDA

Image
   Afisa Miradi wa Shirika la Empower Society Transform Lives (ESTL) linalojishughulisha na utoaji wa huduma ya uelimishaji jamii kuondokana na Ukatili wa kijinsia, ikiwemo ukeketaji, na mila potofu katika Mkoa wa Singida kwa ufadhili wa Ubalozi wa Uholanzi, Annamaria Mashaka, akizungumza na wajumbe wa kamati ya ulinzi wa mwanamke na mtoto (MTAKUWWA)  wa Kata ya Msange wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyofanyika jana Halmashauri ya Wilaya ya Singida.   Afisa Mwezeshaji wa Mwanamke na Maendeleo wa  shirika hilo Edna Mtui, akizungumza katika mafunzo hayo. Afisa Mtendaji wa Kata ya Msange, Clement Jumbe akizungumza katika mafunzo hayo/ Mafunzo yakiendelea. Mjumbe wa Kamati hiyo Sheikh Hassan  Ipande akizungumza katika mafunzo hayo/ Mjumbe wa Kamati hiyo Felister John akizungumza kwenye mafunzo hayo/ Mjumbe wa Kamati hiyo Theresia Yambi akizungumza kwenye mafunzo hayo. Mafunzo yakiendelea. Mafunzo yakiendelea.   Na Dotto Mwaibale, Singida. SHIRIKA la Empower Society Transform Live

SEKTA YA MIFUGO INA MCHANGO MKUBWA KATIKA KUKUZA UCHUMI WA NCHI-PROF.OLE GABRIEL

Image
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza wakati wa hafla ya kuwapatia vyeti wauza wa pembejeo sita waliochaguliwa kushiriki katika kutoa huduma za ugani kwa wafugaji walioko maeneo ya Dar es Salaa, Pwani, Morogoro na Tanga. Mratibu wa Mradi wa AgResults Tanzania Dairly Productivity Challenge Bi.Neema Mrema akizungumza wakati wa hafla ya kuwapatia vyeti wauza wa pembejeo sita waliochaguliwa kushiriki katika kutoa huduma za ugani kwa wafugaji walioko maeneo ya Dar es Salaa, Pwani, Morogoro na Tanga. Mshirika wa Price Water house Cooper (PwC), Bw.Nelson Msuya wakati wa hafla ya kuwapatia vyeti wauza wa pembejeo sita waliochaguliwa kushiriki katika kutoa huduma za ugani kwa wafugaji walioko maeneo ya Dar es Salaa, Pwani, Morogoro na Tanga. Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw.Steve Michael wakati wa hafla ya kuwapatia vyeti wauza wa pembejeo sita waliochaguliwa kushiriki katika kutoa huduma za

COSTECH YAWAALIKA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO KATIKA MAONESHO YA SABASABA

Image
    Mbunifu kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Bw.Yoel Max (kulia) akiwa na mwenzake akionesha moja kadi ambayo inamtambulisha mjasiliamali ambaye atajiunga na programu ya Yu-Sokoni na kutambulika. ******************* Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) inawakaribisha wananchi kwa ujumla kwenye banda lao katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa kwenye viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba jijini Dar es Salaam kujionea teknolojia zilizoibuliwa na Tume hiyo. Akizungumza katika Maonesho hayo Mmoja wa Wabunifu walioibuliwa na Tume hiyo Bw.Yoel Max amesema uwepo wa COSTECH wameweza kusaidia kuibua wataalamu wengi na wabunifu ambao wengi wameweza kujiajiri na kuajiriwa kwenye makampuni makubwa hapa nchini kupitia Teknolojia. Bw.Max ambaye ameweza kubuni programu maalumu ambayo inasaidia kuagiza ama kuuza bidhaa mtandaoni kwa usalama na uhakika na kuweza kuwanufaisha wajasiliamali wengi ambao wanatumia programu hiyo inaiyoitwa Yu-Sokoni. &qu

RAIS SAMIA AIPONGEZA BURUNDI KWA KUADHIMISHA MIAKA 59 YA UHURU

Image
  RAIS wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewapongeza wananchi wa Burundi kwa kuadhimisha miaka 59 ya uhuru wa nchi hiyo huku wakiendelea kudumisha amani. Pia, Mheshimiwa Rais Samia amempongeza Rais wa Burundi Mheshimiwa Evariste Ndayishimiye kwa jitihada zake za kukuza amani, demokrasia na uchumi. Hayo yamesemwa leo (Alhamisi, Julai Mosi, 2021) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipowasilisha salamu za Rais Samia katika sherehe za maadhimisho hayo jijini Bujumbura.Burundi ilipata uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa Ubelgiji Julai 1, 1962. “Nipo mbele yako nikimuwakilisha Rais wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Samia. Rais amenituma nilete salamu zake kwako kwamba anawapongeza sana Wana-Burundi kwa kuendelea kukuunga mkono.”   Waziri Mkuu amesema Mheshimiwa Rais Samia amemuhakikishia Rais wa Burundi kwamba ataendeleza uhusiano wa kindugu na wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizo mbili na pia ameahidi kuitembelea Burundi. Kwa upande wake , Rais wa Burundi Mheshimiwa Ndiyashi

KUTOKA MAGAZETINI LEO IJUMAA JULAI 2, 2021

Image
 

MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA UFUNGUZI WA JUKWAA LA USAWA

Image
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amehudhuria ufunguzi wa Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa (Generation Equality Forum) linalofanyika Paris Ufaransa. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa hilo. Jukwaa hilo lenye madhumuni ya kuchagiza Usawa wa kijinsia linajadili Umuhimu wa uwezeshaji wanawake kiuchumi kama nyenzo ya kumnyanyua mwanamke kwa maendeleo na ustawi wa jamii. Kati ya mambo yaliyojadiliwa katika jukwaa hilo ni kumwezesha mwanamke kupata Teknolojia rahisi na sahihi katika kufanya shughuli za kiuchumi; kutolewa mafunzo ya ujasiriamali pamoja na utoaji wa mitaji kwa wanawake pamoja uwepo wa mifumo sahihi ya kidigitali katika shughuli za kiuchumi zinazofanywa na wanawake. Katika Jukwaa hilo hii leo Julai 1 ,2021 Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango anatarajia kutoa Ahadi za Tanzania kama kinara wa uwezeshaji wanawake kiuchumi kama ilivyoridhiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassa

WAZIRI MKUU KASIM MAJALIWA AWASILI NCHINI BURUNDI KWA ZIARA YA SIKU MOJA

Image
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokelewa na mwenyeji wake, Makamu wa Rais wa Burundi, Prosper Bazombanza, wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Bujumbura, akiwa katika ziara ya siku moja nchini Burundi Julai 01, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Bujumbura na akipokelewa na mwenyeji wake, Makamu wa Rais wa Burundi, Prosper Bazombanza (kulia), akiwa katika ziara ya siku moja nchini Burundi Julai 01, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Makamu wa Rais wa Burundi, Prosper Bazombanza, akiwa katika ziara ya siku moja nchini Burundi Julai 01, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)