Posts

RAIS DKT. MWINYI AKUTANA NA UONGOZI WA ZSSF

Image
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameutaka uongozi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kutambua kwamba madhumuni ya mfuko huo ni kuwasadia wastaafu ili waweze kuishi vizuri baada ya ustaafu wao.   Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo Ikulu jijini Zanzibar wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) ukiongozwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko huo Nassor Shaaban Ameir.   Katika maelezo yake alisema kwamba kuna utofauti mkubwa wa wastaafu wa hapa nchini na nchi nyengine duniani ambapo kwa upande wa nchi hizo wastaafu baada ya kustaafu kazi ndipo huishi vizuri zaidi kuliko wakiwa kazini.   Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa watu wamekuwa wakitoa fedha zao na kuziweka katika Mfuko wa ZSSF katika kipindi  chao chote cha kazi ambapo fedha hizo zimekuwa zikiekezwa kwa miaka mingi hivyo, wamekuwa na matarajio makubwa kwamba watapata faida kubwa baada ya kustaafu lakini kinachotoka ni tofauti.   A

BARRICK-NORTH MARA YATUNUKIWA TUZO KWA KUFANIKISHA UZINDUZI MWA MWONGOZO WA UWEKEZAJI MKOANI MARA

Image
  Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (Kulia) akikabidhi cheti kwa Meneja wa Mahusiano ya Jamii wa mgodi wa Barrick North Mara,Gilbert Mworia, (Kushoto) kutokana na mchango wa kampuni hiyo kufanikisha uzinduzi wa mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa Mara katika hafla iliyofanyika mjini Musoma. Katikati mwenye miwani ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, mhandisi Robert Gabriel Luhumbi. Waziri Mkuu,Mhe. Kassim Majaliwa (Kulia) akikabidhi tuzo kwa Meneja wa Mahusiano ya jamii wa mgodi wa Barrick North Mara, Gilbert Mworia, (Kushoto) kutokana na mchango wa kampuni hiyo kufanikisha uzinduzi wa mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Mara, katika hafla iliyofanyika jana mjini Musoma.Katikati mwenye miwani ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, mhandisi Robert Gabriel Luhumbi. Kampuni ya Barrick ilishiriki pia katika maonyesho hayo *** Kampuni ya Barrick, kupitia mgodi wake wa North Mara, imetunukiwa tuzo kwa  kufanikisha uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji (Investment Guide ) mkoani Mara uliofanyika katika viwanja vya Mwembeni Comple

DKT. NCHEMBA: UPEKUZI WA WATEULE NI ENDELEVU

Image
  Na, Saidina Msangi, WFM, Dodoma. Serikali imesema kuwa  siyo sahihi kuwa na Kanzidata ya  U pekuzi (Benki ya Waliopekuliwa) ili kurahisisha mchakato wa upekuzi kwa kuwa utendaji na mienendo ya  m aafisa hubadilika kuendana na wakati husika . Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), alipokuwa akijibu swali la  M heshimiwa  J erry  W illiam  S il a a , Mbunge wa  Ukonga   alieitaka Serikali  kuanzisha Benki ya waliopekuliwa  kwa ajili ya uteuzi  ili  kurahisisha zoezi la uteuzi wa Bodi za  Taasisi  na kuziwezesha Taasisi  hizo kwenda na kasi ya Mhe. Rais kwa  kile alichosema kuwa  upekuzi  u mekuwa kisingizio cha kuchelewesha uteuzi . “U pekuzi kwa ajili ya kujaza nafasi mbalimbali hufanyika kwa wakati husika kutokana na ukweli kwamba utendaji na mienendo ya maafisa pia hubadilika kutoka wakati mmoja hadi mwingine ,”   ali fafanua  Mhe.  Nchemba . Aidha, alieleza kuwa  Wizara ya Fedha na Mipango ina jumla ya Taasisi 28

ZIARA YA RAIS SAMIA SOKO KUU LA KARIAKOO, DAR ES SALAAM

Image
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan afanya ziara ya Kushtukiza katika Soko Kuu la Kariakoo Jijini Dar es Salaam Juni 1, 2021.(Picha na Ikulu).  

MAJALIWA: TUMIENI NISHATI MBADALA

Image
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameziagiza Wizara, Taasisi, Mashirika yote ya Serikali na Sekta Binafsi pamoja na vikundi vya uzalishaji zinazotumia nishati ya kuni na mkaa zianze kutumia nishati mbadala kwa  kupikia na shughuli nyingine za uzalishaji. Ametoa wito huo leo (Jumanne Juni Mosi, 2021) wakati akitoa tamko kuhusu Wiki ya Mazingira Duniani, katika ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma. Amesema kuwa taasisi kama shule, vyuo, hospitali na majengo makubwa  zinapaswa kuzingatia ufungaji wa mifumo ya nishati ya gesi kwa ajili ya kupikia. “Kila Wizara ifanye ufuatiliaji kwenye taasisi zake na nipatiwe taarifa ya hali ya utekelezaji kila baada ya miezi sita inayoonesha ni taasisi ngapi zimefikiwa, zimebadili mifumo au zimejenga majengo kwa kuzingatia hitaji la nishati mbadala” “Suala la uhifadhi, utunzaji, usimamizi na usafi wa mazingira lisiwe jambo linalofanyika wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani pekee, bali tujenge tabia ya kuliona kwamba ni suala la kila siku” amesisitiza

WABUNGE WASHAURI SOMO LA SAYANSI KIMU KUREJESHWA SHULENI

Image
Shirika lisilo la Kiserikali la Agri Thamani Neema Lugangira ambaye pia ni MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo WABUNGE wameishauri Serikali kurudisha mashuleni somo la sayansi kimu ili watoto wafundishwe kuandaa lishe bora tangu wakiwa watoto, jambo ambalo litasaidia kupambana na athari zitokanazo na lishe duni. Akizungumza katika semina lishe kwa Umoja wa Wabunge Wanawake (TWPG), iliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Agri Thamani, Mbunge wa Urambo (CCM) Magareth Sitta alisema zamani watoto walifundishwa juu ya kutayarisha chakula lakini hivi sasa hawajifunzi tena. “Serikali kwanini wameondoa somo la domestic sience (sayansi kimu) sisi wengine tulijifunza kule namna ya kuandaa chakula. Na kwanini wanafunzi hawana mashamba ya shule,”alisema. Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Anna Lupembe aliunga mkono kauli ya Sitta ambaye alitaka wataalam wa lishe kutembea katika halmashauri kwa ajili ya kutoa elimu y

WIZARA ZA KISEKTA ZAKUTANA NA WAZIRI WA FEDHA KUJADILI BAJETI KUU YA SERIKALI

Image
Na, Josephine Majura, WFM, Dodoma Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya Mawaziri wa Sekta mbalimbali na kuwahakikishia kuwa maeneo yote ya kipaumbele yatazingatiwa ili kuchochea maendeleo ya nchi kupitia miradi itakayotekelezwa na Wizara hizo. Dkt. Nchemba alisema kuwa lengo la kikao hicho lilikuwa ni kujadili na kupitia maeneo ya vipaumbele kwenye kila sekta ili kuona kama yamejumuishwa kwenye hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kabla ya kusomwa Bungeni Jijini Dodoma Juni 10 mwaka huu. “Nimekutana na viongozi mbalimbali ili kupunguza mazingira yaliyokuwa yakijitokeza nyuma kwamba maeneo ya vipaumbele vya Sekta fulani hayajawekwa sawa”, Alisema Dkt. Nchemba. Aliongeza kuwa maeneo mengi ya vipaumbele yamekuwa yakiwekwa tofauti na matakwa ya Wizara na Sekta husika hivyo kikao hicho kilikaa ili kubainisha maeneo ya vipaumbele ambayo hayakujumuishwa kwenye Bajeti Kuu na kuangalia uwezekano wa kuyajumuisha kama ilivyopen