MAKAMU WA RAIS MTEULE AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
Na Josephine Majura na Farida Ramadhani, WFM, Dodoma. Makamu wa Rais Mteule, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, amekutana na Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango na kuwasisitiza kuendelea kufanya kazi kwa bidii kutokana na umuhimu wa Wizara hiyo katika maendeleo ya nchi. Mheshimiwa Philip Isdor Mpango, ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango, alitoa rai hiyo jijini Dodoma alipokutana na watumishi wa Wizara hiyo katika ofisi zilizopo Treasury Square, akitokea bungeni baada ya kuteuliwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Bunge kuthibitisha uteuzi wake kwa kura za kishindo. Dkt. Mpango amewataka watumishi wa wizara hiyo kuendelea kufanya kazi kwa weledi kwa kuwa wizara hiyo ni moyo wa Serikali na kwamba wasipofanya kazi vizuri na kwa uaminifu hakuna miradi ya maendeleo itakayotekelezwa, mishahara haitapatikana wala mikopo itakayokopwa hivyo kukwamisha maendeleo ya wananchi. Alisema hana shaka na uwezo wa viongozi na wataalam