WAZIRI SIMBA HAWENE AWASWEKA RUPANGO VIONGOZI WA VIJIJI KWA KUSHAWISHI VURUGU WAFUGAJI, WAKULIMA KITETO
Na Mwandishi Wetu, MOHA, Kiteto_ WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene ameamuru kukamatwa na kuwekwa mahabusu viongozi wa vijiji vya Miriongima na Kijungu Wilayani Kiteto kwa kosa la kushawishi wananchi kufanya vurugu na kuvamia eneo lililotengwa na Serikali kwa shughuli za mifugo. Akizungumza katika mkutano wa hadhara na Wananchi wa Kitongoji cha Miriongima, Kijiji cha Kijungu, Wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara, leo, Waziri Simbachawene alisema viongozi hao wa vijiji ndio wanaochochea migogoro ambayo inaendelea kwasababu wanawadanganya wananchi na kupelekea kuvamia maeneo ambayo yametengwa kwa shughuli za mifugo kwa kufanya kilimo kinyume na utaratibu. “Nimekuja kwasababu ya uvunjifu wa amani, nimekutana na viongozi wenu wa Wilaya na Mkoa, pia nimetembelea Kijiji cha Amei, na nyie hapa nimewasikiliza, kwa wale ambao mlienda kulima kule ardhi ya Kijiji cha Amei, mkiamini kwamba viongozi hawa wa Kijiji cha Kijungu ni wakweli, sasa muelewe kuanzia leo kwamba wamewadanga