SERIKALI IMETENGA MEGAWATI 70 ZA UMEME KUENDESHA TRENI YA MWENDOKASI, DKT. KALEMANI ASEMA HATA LEO TRENI IKIWA TAYARI UMEME UPO.
NA K-VIS BLOG, MOROGORO WAZIRI wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani amesema Serikali kupitia TANESCO tayari imetenga Megawati 70 za umeme wa kuendesha treni ya mwendokasi maarufu SGR. Mhe. Dkt. Kalemani ameyasema hayo leo Februari 27, 2021 wakati akifungua rasmi kikao kazi cha TANESCO na Wahariri wa vyombo vya habari kwenye ukumbi wa NSSF mkoani Morogoro. Mahitaji halisi ya kuendesha treni hiyo ya umeme ni Megawati 27. “Tunampongeza sana Rais wetu kwa kuamua kujenga SGR, hata treni hiyo ingekuwa tayari leo treni hiyo ingeendeshwa kwa umeme bila mashaka yoyote.” A.lisisitiza. Alisema tayari miundombinu ya umeme kiasi cha kilomita 160 ikiwa ni pamoja na kuweka nguzo na nyaya za umeme kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro imekamilika na kwamba kinachosubiriwa ni kuiunganisha treni hiyo na umeme wa TANESCO. Akizungumzia hali ya umeme nchini kwa sasa, Mhe. Waziri amewahakikishia watanzania na wawekezaji wa ndani na nje kuwa umeme wa kuhakikisha unaendesha uwekezaji wao upo wa kutosha na wa uha