Posts

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMANNE FEBRUARI 2, 2021

Image
 

WAGANGA WAKUU IMARISHENI MIFUMO YA UDHIBITI NA KINGA YA MAGONJWA: Dkt. GWAJIMA

Image
*Wizara haina mpango wa kupokea chanjo ya COVID-19 Na. Catherine Sungura, WAMJW-Dodoma Waganga Wakuu wa Mikoa, Wilaya,Wafawidhi na Maafisa Afya Mazingira nchini  wametakiwa kuendelea kuimarisha mifumo yote ya udhibiti na kinga ya magonjwa kwa kushirikiana na wananchi ili kudhibiti magonjwa  yote ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza. Rai hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima wakati akitoa ufafanuzi juu ya maswali ya wanahabari kuhusu kujikinga na magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ambukiza kwenye ukumbi wa wizara jijini Dodoma. Dkt. Gwajima amesema viongozi hao wanatakiwa kuwakumbusha wananchi kwenye elimu ambayo Wizara imekuwa ikiitoa ikiwemo kuimarisha usafi, kujifukiza, kufanya mazoezi, kula lishe bora, kunywa maji mengi bila kusahau matumizi ya tiba asili ambazo taifa hili limejaaliwa. “Serikali itaendelea kuchukua tahadhari zote za ufuatiliaji wa mwenendo wa magonjwa yote kama ambavyo imekuwa ikifanya siku zote na kuen

RAIS MAGUFULI AHUTUBIA KILELE CHA SIKU YA SHERIA NA MIAKA 100 YA MAHAKAMA KUU

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Viongozi mbalimbali, Wafanyakazi wa Mahakama, Majaji pamoja na wananchi wa mkoa wa Dodoma katika kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini na miaka 100 ya Mahakama Kuu yaliyofanyika katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma leo tarehe 1 Februari 2021. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Viongozi mbalimbali, Wafanyakazi wa Mahakama, Majaji pamoja na wananchi wa mkoa wa Dodoma katika kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini na miaka 100 ya Mahakama Kuu yaliyofanyika katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma leo tarehe 1 Februari 2021. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma akizungumza cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini na miaka 100 ya Mahakama Kuu yaliyofanyika katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma leo tarehe 1 Februari 2021. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli

STARA THOMAS, HAFSA KAZINJA KUKABIDHIWA KADI ZA MATIBABU NA WAZIRI BASHUNGWA

Image
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa.  Wanamuziki Stara Thomas na Hafsa Kazinja wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Eric Kisanga (kushoto) na Katibu Mkuu wa umoja huo, Stella Joel  (kulia) baada ya kufanya mazungumzo jijini Arusha juzi kuhusu Kongamano la Fursa kwa wanamuziki litakalofanyika Februari  20, 2021 Jijini humo.   Na Dotto Mwaibale. WANAMUZIKI Maarufu  Nchini Stara Thomas na Hafsa Kazinja ni miongoni mwa baadhi ya wanamuziki watakao pata kadi za bima ya afya ya Taifa (NHIF) zitakazotolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa. Bashungwa ambaye atakuwa mgeni rasmi atatoa kadi hizo katika Kongamano la Fursa kwa wanamuziki litakalofanyika Februari  20, 2021 Jijini Arusha.   "Mastaa hawa Stara Thomas na Hafsa Kazinja tayari wametimiza vigezo vya kupata kadi hizo za bima ya afya baada ya  kukutana na Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Eric Kisanga na Kati

WATUMISHI HESLB WAPATIWA MAFUNZO YA UWEZO KUWAJENGEA

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru. Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Neema Kuwite akizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa ofisi hiyo katika kusimamia na kutekeleza majukumu yao yaliyohimishwa jana (Jumapili Januari 31, 2021). Mafunzo hayo ya siku mbili yalifanyika tarehe 30-31 Januari mwaka huu Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Neema Kuwite akizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa ofisi hiyo katika kusimamia na kutekeleza majukumu yao yaliyohimishwa jana (Jumapili Januari 31, 2021). Mafunzo hayo ya siku mbili yalifanyika tarehe 30-31 Januari mwaka huu Jijini Dar es Salaam. Watumishi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wakifuatilia kwa makini mafunzo elekezi yaliyotolewa na wakufunz