KATIBU TAWALA MKOA WA SINGIDA ATOA MAAGIZO MAZITO KWA SEKTA YA ELIMU
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dk. Angelina Lutambi, akizungumza na wakuu wa shule za sekondari na maafisa elimu kata katika kikao kazi kilichofanyika jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Shule ya Sekondari Mwenge mkoani hapa. Afisa Elimu Mkoa wa Singida, Nelasi Mulungu, akizungumza kwenye kikao hicho. Kikao kikiendelea. Na Mwandishi Wetu, Singida KATIBU Tawala Mkoa wa Singida Dk. Angelina Lutambi amewataka wakuu wa shule na maafisa elimu kata mkoani hapa kufanya kazi kwa bidii ili kubadilisha mitazamo ya jamii zinazozunguka shule zao. Lutambi aliyasema hayo jana katika kikao kazi cha wakuu wa shule zote za Sekondari na maafisa elimu kata kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Shule ya Sekondari Mwenge ambacho kililenga kufanya tathimini ya matokeo ya kidato cha nne na kidato cha pili Mwaka 2020. Katibu Tawala huyo alisema wakuu wa shule ni chachu ya mabadiliko kwenye jamii inayowazunguka ,wanafunzi wanapomaliza shule na kurudi kwa jamiii hivyo kama jamii haijabadilika ni isha