Posts

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMATATU JANUARI 4, 2021

Image
 

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAPILI JANUARI 3, 202I

Image

WAZEE WASTAAFU WATEMBELEA MRADI WA UMEME WA JULIUS NYERERE WA MEGAWATI 2115 NA KUTOA NENO KWA VIJANA WA KITANZANIA

Image
 Na mwandishi wetu, JNHPP WAZEE ni hazina ya Taifa na kuna msemo wa Kiswahili usemao “Uzee ni Dawa”,   Januari 2, 2021 Wazee Wastaafu kutoka Chama cha Saidia Wazee Tanzania (SAWATA) walipata fursa ya kutembelea mradi mkubwa wa kimkakati wa Umeme wa Maji wa Julius Nyerere (JNHPP 2115) unaotekelezwa kwenye bonde la mto Rufiji na kutoa neno “Vijana mlioko hapa muwe waadilifu”. Kilichopelekea kutolewa kwa neno hilo ni jinsi wazee hao walivyostaajabishwa na jinsi ujenzi wa bwawa hilo unavyotekelezwa kisasa tena asilimia zaidi ya 90 ni vijana wa Kitanzania ndio wametawala eneo hilo la kazi. “Tumefurahi kuwa sehemu ya mradi huu, kwa sababu hiki ni chanzo kikubwa cha kuelimisha watoto wetu, tumeona local content, watanzania wanaoshiriki katika ujenzi wa mradi huu ni wengi kwa hiyo capacity building inafanyika ipasavyo naomba tuendelee mujenga uchumi wetu na tuendelee kuijenga nchi yetu.” Alisema Balozi mstaafu Nyasugara Kadege ambaye alikuwa ni miongoni mwa wazee hao waliotembelea eneo h

WAZIRI KALEMANI AIGIZA TANESCO KUWAOMBEA AJIRA WATUMISHI WALIOAJIRIWA KWA MIKATABA YA MUDA MFUPI KWA KIPINDI KIREFU.

Image
Na Dorina G. Makaya - Shinyanga. Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani, ameliagiza Shirika la TANESCO nchi nzima, kuwaombea ajira watumishi walioajiriwa kwa vipindi vifupi na kuitumikia TANESCO kwa muda mrefu. Waziri Kalemani ametoa agizo hilo tarehe 30 Mwezi Desemba, alipokuwa akizungumza na watumishi wa TANESCO wa Mkoa wa Shinyanga, katika kikao kazi cha kufahamiana, kusikiliza kero na kutoa maelekezo ya kazi ili kuliwezesha shirika la TANESCO nchini kufanya kazi kama timu moja kwa kasi kwa ubunifu na kwa usahihi ili kufikisha huduma ya umeme kote nchini na kuongeza mapato ya Serikali kutokana na Sekta ya Nishati. Akizungumza baada ya kusikiliza Kero za Watumishi wa TANESCO mkoa wa shinyanga, Waziri Kalemani ameweka bayana kuwa, watumishi hao wanaoajiriwa kwa vipindi vifupi ndio wanaokutana na wateja moja kwa moja na kujenga taswira ya TANESCO (Visibility) kwa wateja wanaohitaji na kutumia huduma ya umeme hapa nchini. Amesema, kufanya kazi kama kibarua kwa miaka mingi bila ya k

MTOTO WA BABA WA TAIFA, ROSEMARY NYERERE AFARIKI DUNIA

Image
Rosemary Nyerere (pichani) ambaye ni mtoto wa hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarqge Nyerere amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Januari 2, 2021 jijini Dar es salaam. Taarifa zilizopatikana hazikufafanua zaidi lakini  Msiba upo nyumbani kwa Mwalimu huko Msasani.

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAMOSI JANUARI 2, 2020

Image