DKT. NDUGULILE AZIPA SIKU 30 TAASISI ZA UMMA ZINAZODAIWA NA TTCL KULIPA MADENI
Na Prisca Ulomi, WMTH Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile amezipa siku 30 taasisi za umma zinazodaiwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kulipa madeni kwa Shirika hilo ili liweze kujiendesha, kutekeleza majukumu yake ya kutoa huduma ya mawasiliano ya sauti na data kwa taasisi za Serikali, sekta binafsi na wananchi ili kukuza uchumi na kuchangia pato la taifa. Dkt. Ndugulile ameyasema hayo wakati wa ziara yake alipotembelea TTCL kwa lengo la kufahamiana na kuzungumza na wajumbe wa Bodi, Menejimenti na wafanyakazi wa TTCL, Dar es Salaam ambapo aliambatana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Kundo A. Mathew na Mejimenti ya Wizara hiyo Ameongeza kuwa zaidi ya taasisi 20 za Serikali zinadaiwa na TTCL zaidi ya kiasi cha shilingi bilioni 30 ambapo zipo taasisi zinatumia huduma za mawasiliano za TTCL na zinakusanya mapato ya zaidi ya shilingi bilioni moja kwa mwezi ila hawako tayari kulipa huduma za TTCL Vile vile, ametoa onyo kali kwa kampuni zin