Posts

PINDA:KILIMO PEKEE NDICHO KITAONDOA UMASIKINI TANZANIA.

Image
  Katibu wa Chama cha Wachumi Kilimo Tanzania (AGREST) Dkt. Betty Waized akitoa salamu za Chama hicho na malengo ya mkutano huo kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kwaajili ya ufunguzi.  Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Mizengo Pinda akitoa nasaha zake mbele ya Wataalamu hao wa Uchumi Kilimo wakati akifungua rasmi mkutano huo wa 12 wa Kisayansi wa  Chama hicho mjini Dodoma. Profesa. Aida Isinika akimkabidhi Pinda zawadi maalumu iliyotolewa na chama hicho kama kumbukumbu. Mkutano ukiendelea. Mkutano ukiendelea. Mkutano ukiendelea. Wanachama wa AGREST na Mgeni rasmi Mizengo Pinda mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo wa 12 wa kisayansi. Washiriki wa mkutano wakifuatilia hotuba za ufunguzi. Washiriki wa mkutano wakifuatilia hotuba za ufunguzi.  Na Calvin Gwabara, Dodoma Imeelezwa kuwa Tanzania haitaweza kuondoa umasikini wala kupiga kasi ya Kim aendelee kwa Wananchi wake endapo swala la Kilimo Bora na cha kisasa halitapewa kipaumbele na Serikali, Watafiti na wadau wengine wa kilimo. Hayo yam

DPP Afafanua Alivyomtoa Gerezani Kada CHADEMA Nusrat Hanje

Image
  Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), Biswalo Mganga ametoa ufafanuzi kuhusu kumfutia mashitaka kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Nusrat Hanje ambaye alivuliwa uanachama Novemba 27 mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa habari, Biswalo amesema kesi ameifuta yeye kwa mamlaka aliyonayo kisheria chini ya kifungu cha 91 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai. Amesema wanaolalamika kuwa amemfutia kesi kada huyo kinyume na taratibu wanakiuka utaratibu . Biswalo amesema sheria ipo na inafanyakazi zake na hakuna kufanya kazi kwa upendeleo.

TANESCO YAWAPANDISHA KIZIMBANI WATU SABA KWA KUINGILIA MIUNDOMBINU YA UMEME

Image
Watu Saba wakazi wa Ukonga, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na kesi ya uhujumu Uchumi kwa kuisababishia hasara Tanesco Washtakiwa hao ni  Mwalimu Boniphace Singaille(48) Twalibu Kasamu(32), Mwarami Mussa(45), Vumilia Kambi na Haidary Hassan (35). Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali Mkuu, Materus Marandu akisaidianaia na Kija Luzungana,  mbele ya hakimu  Mkazi Mkuu  Kassian Matembele. Wakili Marandu alidai, washtakiwa kwa pamoja na wenzao wawili ambao ni wagonjwa wanadaiwa January 2018 eneo la Kichangani Ukonga Madafu,  waliingilia miundombinu inayotumika kutoa huduma muhimu kwa kutoa  mita ya Tanesco kutoka katika kiboksi kinachohifadhia mita na kuifunga moja kwa moja. Pia, kati ya Januari  18 na Agosti 2020 katika eneo hilo, washitakiwa wote kwa makusudi waliingilia mita ya umeme wa Tanesco na hivyo kuisababishia shirika hilo hasara ya Sh 6,868,910. Upande wa mashtaka ulidai upelelezi haujakamilika na kwamba wanaomba tarehe ny

AIRTEL YAJA NA OFA YA SIKUKUU WATEJA KUPEWA DABO DATA

Image
Mkuu wa Kitengo cha Data kampuni ya Simu za mkononi, Airtel, (kulia) na Meneja Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Jackson Mbando wakizindua rasmi Ofa ya Siukuu kwa wateja kwa kuwapa Dabo Data   Dar es Salaam, :  Kampuni ya simu za Mkononi Airtel Tanzania leo imetangaza kuzindua ofa ya  Airtel Smartphone Dabo Data  kwa wateja wote wa simu aina ya Smartphone kwa msimu huu wa sikukuu. Pia ofa hii itawanufaisha Wateja wote wa sasa wa Airtel wanyempango wa kubadilisha simu au Smartphone mpya kwa kujipatia Dabo Data kwa bando za wiki na mwezi kwa miezi sita ijayo yaani nusu mwaka. Airtel inapozindua Ofa hii ya shamrashamra za mwisho wa Mwaka Wateja wengine wa smartphone kwa sasa wanaweza kujiunga na mtandao wa Airtel ili kufurahi ofa hii. Ofa hii ni pale mtu mtumiaji wa simu aina ya smartphone anapotumia mtandao wa Airtel kwa mara ya kwanza kwenye simu yake. Ofa hii inatoa fursa kwa wateja kufurahia huduma yenye kasi ya Airtel 4G inayopatikana nchini kote Tanzania.    Ofa ya Dobo Data inampa mteja

MBUNGE WA BUYUNGU ATOA MSAADA WA MABATI 300 KUSAIDIA SHULE ZA SEKONDARI

Image
   Mbunge wa Jimbo la Buyungu mkoani Kigoma kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Aloyce Kamamba (katikati kushoto), akikabidhi bati moja kati ya 300  kwa ajili ya ujenzi wa shule za sekondari jimboni humo. Mkuu wa wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala (kushoto) akikabidhiwa mifuko ya saruji 100 na Kampuni ya Ujenzi ya Nyanza Road kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Kanyonza Moja ya madarasa ya shule za sekondari jimboni humo.   Na Mwandishi Wetu, Kigoma. MBUNGE  wa Jimbo la Buyungu mkoani Kigoma kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Aloyce Kamamba, amekabidhi mabati 300 yenye thamani ya sh.milioni 9 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni. Akizungumza katika hafla ya kukabidhi mabati hayo, Kamamba alisema ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni ya kutatua changamoto mbalimbali. "Niliahidi kutatua changamoto mbalimbali za wananchi katika jimbo letu na nimeanza na changamoto za miundombinu kwa kununua mabati  300 kwa ajili ya ujenzi wa shul

RC KUNENGE AGEUKA MBOGO, NI BAADA YA KUJIONEA "UBABAISHAJI" KWENYE JARIBIO LA KWANZA LA UCHINJAJI WA NG'OMBE NA MBUZI MACHINJIO YA VINGUNGUTI

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge ameonyesha kutoridhishwa na zoezi la majaribio ya uchinjaji wa Ng'ombe na Mbuzi kwenye machinjio ya kisasa Vingunguti baada ya kubaini kasoro za uendeshaji wa mtambo hiyo. Miongoni mwa kasoro alizobaini RC Kunenge ni pamoja kukosekana kwa utaalamu wa uendeshaji wa mitambo, Zoezi la uchinjaji kutumia muda mrefu kuanzia hatua ya Kwanza Hadi mwisho, kukwamakwama kwa vifaa kwa baadhi ya maeneo, Kazi nyingi kufanywa na binadamu badala ya mashine Na  wafanyakazi kufanya kazi kwa kubahatisha jambo lililopelekea Ng'ombe mmoja kutumia zaidi ya nusu saa Hadi kukamilika badala ya dakika 10. Kutokana na hayo RC Kunenge amemtaka Mkandarasi wa ufungaji wa mashine, Mshauri wa Mradi, NHC na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kufika ofisini kwake Alhamis ya Disemba 3 saa nne asubuhi. Aidha RC Kunenge amewaelekeza NHC kuongeza kasi ili Ujenzi wa jengo ukamilike kwa wakati huku akimuelekeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuwa mkali. Pamoja na hay

RC KUNENGE KUKUTANA NA WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI DAR DISEMBA 10.

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge (pichani juu) anatarajia kukutana na Wafanyabiashara na Wawekezaji Jijini humo mnamo Disemba 10 Mwaka huu kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere posta. RC Kunenge amesema lengo la mkutano huo ni kuweka mazingira Bora ya Uwekezaji na biashara ili kila mmoja aweze kunufaika na shughuli anayoifanya. Aidha RC Kunenge amesema kupitia mazingira Bora ya Biashara na Uwekezaji itarahisisha ukusanyaji mzuri wa Kodi na ongezeko la ajira kwa wananchi.