Posts

JENERALI MABEYO ATUNUKIWA NISHANI MAALUM YA MLIMA KILIMANJARO

Image
Chuo Kikuu cha Iringa (zamani Tumaini University) kimemtunukia Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Salvatory Venance Mabeyo (pichani juu) Nishani Maalum ya Mlima Kilimanjaro (University of Iringa Miunt Kilimanjaro Award) ambayo hutolewa kwa Viongozi wa juu Serikalini ambao wametoa mchango wa kutukuka kwa Chuo au Tasnia ya Elimu kwa ujumla. Tukio hilo limefanyika wakati wa Mahafali ya 23 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika "campus" ya Chuo Mjini Iringa tarehe 28 Nov 20. Mwingine aliyetunukiwa Nishani hiyo Maalum ya juu wakati wa Mahafali hiyo ni Mkurugenzi wa TAKUKURU, Brigedia jenerali John Julius Mbungo. Kwa mara ya kwanza Nishani hiyo ilitunukiwa kwa aliyekuwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa wakati wa Mahafali ya 22 ya Chuo hicho mwaka 2019. Jenerali Salvatory Venance Mabeyo  Brigedia jenerali John Julius Mbungo  

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMATATU NOVEMBA 30, 2020

Image
 

TANESCO MSHINDI WA JUMLA MASHINDANO YA SHIMMUTA

Image
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeibuka mshindi wa jumla katika mashindano ya SHIMMUTA baada ya kunyakua vikombe tisa na kuibuka kidedea katika mashindano hayo ya michezo ya mwaka 2020, yanayofanyika Mkoani Tanga. Matokeo hayo yanaifanya TANESCO kuwa mshindi wa jumla katika mashindano ya SHIMMUTA mwaka huu yaliyomalizika Mkoani Tanga. Michezo ambayo TANESCO imeibuka na ubingwa ni wavu wanaume na wanawake, kikapu wanaume na wanawake. Aidha, TANESCO imekuwa mshindi wa pili mchezo wa pete. Hii ni mara ya nne mfululizo timu ya kikapu wanaume wanakuwa washindi, na mara ya pili mfululizo kwa timu ya wavu wanaume inaibuka na ushindi.  Kwa upande wa michezo ya jadi TANESCO imeshinda mchezo wa bao wanawake, karata wanaume na mshindi wa pili bao kwa wanaume.  Mbali ya vikombe hivyo, TANESCO pia imepata medali saba ambapo Polycaps Ernest amekuwa mahindi wa tatu mbio za mita 100 na mita 200, Kulwa Mangala mshindi wa pili mita 1500, Grace Moshi mshindi wa pili mita 400 na 800, mshindi wa tatu

MAONYESHO YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI YAZINDULIWA SHINYANGA

Image
  Mgeni Rasmi mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, akizungumza kwenye maonyesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoani Shinyanga. Eneo la maonyesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoani Shinyanga, lililopo eneo la Butulwa Kata ya Old -Shinyanga. Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akisoma taarifa kwenye maonyesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini. Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi, akisoma taarifa ya maonyesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini. Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi, akizungumza kwenye maonyesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoani Shinyanga. Mwenyekiti wa Chemba ya wafanyabiashara na viwanda mkoani Shinyanga Meshack Kulwa, akitoa shukrani kwenye maonyesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini. Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, (wa tatu kutoka kulia) akizindua maonyesho ya Biashara na Teknolojia ya madini mkoani Shinyanga, wapili kulia ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zain

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAPILI NOVEMBA 29, 2020

Image