LATRA YATANGAZA NAUALI MPYA YA TRENI MOSHI-ARUSHA
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza nauli za treni ya abiria itakayofanya safari zake kutoka Moshi mjini hadi Arusha na kurudi Moshi. Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Arusha leo tarehe 29 Septemba, 2020, Mkurugenzi Mkuu wa LATRA Gilliard Ngewe amesema nauli hizo zimetangazwa kufuatia Shirika la Reli Nchini (TRC) kuwasilisha maombi ya nauli hizo, ambapo LATRA ilifanya mikutano ya kupokea maoni ya wadau, kisha kufanya uchambuzi wa maoni hayo pamoja na kuchambua mchanganuo uliowasilishwa na TRC. Kwa mujibu wa kifungu cha 21 (2) (b) cha Sheria ya LATRA namba 3 ya 2019, baada ya mchakato wa uchambuzi kukamilika, Bodi ya Wakurugenzi ya LATRA imeidhinisha nauli hizo na kuainisha nauli zitakazotumika kwa usafiri wa treni ndani ya mikoa hiyo na nje ya mikoa kama inavyoonekana katika jedwali. Nauli zilizoidhinishwa na LATRA zikionesha mchanganuo wa vituo vya ndani nan je ya mikoa husika KUTOKA MOSHI KWENDA Umbali (KM) NAULI KWA MADARAJA HUSIKA (SHS): Daraja la tat