Mkuu
wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge amesema lengo la mkoa wake ni kuwa na
mabaraza ya ardhi kwenye wilaya zote za mkoa huo.
Mhe.
Kunenge ameyasema hay oleo Septemba 21, 2021 mwanzoni mwa ziara yake ya
kutembelea wilaya zote za mkloa huo ili kusikiliza kero mbalimbali za wananchi
na kuzipatia ufumbuzi.
Kituo
cha kwanza cha ziara yake kilikuwa ni Wilayani ya Bagamoyo Kata ya Magomeni ambapo
moja ya kero kubw aliyokutana nayo kutoka kwa wananchi ni kutokuwa na baraza la
Ardhi la Wilaya.
Akijibu
kero hiyo RC Kunenge alisema “Mpango wa Mkoa ni kuwa na Mabaraza ya Ardhi katika Wilaya zote kwenye
mkoa wetu, na kwakweli tumeshaunda
Mabaraza hayo kwenye Wilaya za Kibaha na
Mafia,” alisema na kuongeza …………….Wajumbe
wa baraza katika Wilaya ya Mkuranga wataapishwa Jumatano hii, Wilaya ya Kisarawe
Wajumbe wataapishwa Jumatatu wiki ijayo.”
Alibainisha.
RC
Kunenge alisema kwa upande wa Wilaya za Rufiji
na Bagamoyo tayari Mkoa umewasilisha majina ya Wajumbe waliopendekezwa kwa Mhe.
Waziri wa Ardhi na wanasubiri kurejeshewa ili waaendelee na teuzi.
Mhe
Kunenge ameeleza kuwa ziara yake itapita kata kwa kata katika Halmashauri zote
za Mkoa wa Pwani kukagua Miradi na Kusikiliza Kero za Wananchi.
Aidha
Mhe. Kunenge amewahimiza Wananchi kuheshimu sheria ili kumaliza migogoro ya
Ardhi Mkoani hapo.
RC
Kunenge pia amepongeza kukamilika kwa mradi wa Ujenzi wa shule ya Mchepuo wa
kingereza, Kigongoni uliogharimu
Shilingi Milioni 70, ambapo kati ya fedha hizo Tsh Mil 20 zimetokana na nguvu
za wananchi na Tsh Mil 50 Fedha kutoka Serikali Kuu, amewata waalimu kusimamia
taaluma ya Wanafunzi hao ili wafanye vizuri bora kwenye masomo yao.
"Mkurugenzi
shule hii usiiache andaeni mpango mzima master plan wa shule"
Mkoa
wa Pwani umeendelea kuanzisha Shule za
Mchepuo wa Kingereza ambapo mpaka Sasa shule mbili za Serikali za Mchepuo wa
kingereza Kigongoni English medium pre and Primary School Iliyopo Bagamoyo na Mkoani Pre Primary School
Iliyopo Kibaha Mjini zimeanzishwa.
0 comments:
Post a Comment