SEMINA YA WASTAAFUU WATARAJIWA PSSSF YAFANYIKA MWANZA
*RC: Wekezeni katika miradi rafiki
*Msikurupuke kuanzisha miradi, jifunzeni kwanza
*Aipongeza PSSSF kwa semina
Na Mwandishi Wetu,
Mwanza
MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.
Mhandisi Robert Gabriel amewashauri Wastaafu watarajiwa wa Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kuwekeza katika miradi waliyoizoea ili
waweze kuindesha vyema na kwa faida.
Mhandisi Gabriel alisema hayo
Jijini Mwanza wakati wa ufunguzi wa Semina ya Wastaafu watarajiwa kwa wanachama
wa PSSSF wa mkoa wa mwanza inayofanyika Julai 26 hadi 27, 2021.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi Robert Gabriel, akihutubia wakati akifungua semina ya Wastaafu watarajiwa wa PSSSF. Kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa PSSSF, Bi. Beatrice Musa-Lupi na katika ni Bi. Nyamisinda Manyunyi kutoka NMB.
“Kama unataka kuingia katika mradi
wowote, hakikisha unaonana na wataalamu ili waweze kukusaida katika
uwekeza sahihi na wenye tija,” alisauri Bw. Gabriel
Aliwashauri wastaafu hao watarajiwa
watakapolipwa mafao yao wasikurupuke kuanzisha miradi bali yajifunze vyema
mradi wanaotaka kuwekeza ili wajue njia sahihi ya kuwekeza katika mradi huo
“PSSSF wameletea Mabenki na Taasisi
mbalimbali ili muweze kupata uelewa na maarif ili mfanye maamuzi sahihi ya
uwekezaji. Hivyo tumieni fursa vyema, hii bahati kubwa kwenu, kwani sio wote
wanaopata fursa kama hii,” alisema Mkuu wa mkoa wa Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Mhandisi Robert Gabriel (Wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Taasisi za fedha zinazoshiriki semina ya Wastaafu watarajiwa wa PSSSF mkoa wa Mwanza.
Alisema ofisi ya Mkuu wa mkoa wa
Mwanza itatoa elimu na ushauri bure katika kuhakikisha Wastaafu wa mkoa wa Mwanza
wanafanya uwekeza sahihi kwa maslahi yao na taifa kwa ujumla.
Akizungumza awali wakati
akimkaribisha Mkuu wa mkoa wa mwanza, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu ambaye ni
Mkurugenzi wa Fedha Bi. Beatrice Musa-Lupi alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa
kukubali mwaliko wa kufungua semina hiyo kwa wastaafu wa mkoa wa Mwanza.
Wastaafu watarajiwa wa Mkoa wa Mwanza, wakimsalimia Mkuu wa mkoa wa Mwanza (hayupo pichani)
Azishukuru taasisi za fedha
zikizofanikisha kufanyika kwa semina hiyo, taasisi hizo ni CRDB, NMB, TCB, NBC,
DCB, BENKI ABC, BENKI YA AZANIA, MCB na UTT AMIS. Alizishukuru pia kwa kutoa
elimu mbalimbali kwa wastaafu watarajiwa wa PSSSF. Taasisi nyingine
zinazotarajiwa kutoa elimu ni SIDO, TAKUKURU na TCRA.
Akizungumzia semina hizo kwa wastaafu, Bibi Musa-Lupi alisema, “Semina hizi ni endelevu, na zitaendeshwa kila mwaka kwa wanachama wa PSSSF waliobakiza kipindi kisichozidi miaka miwili kabla ya kustaafu.
Comments
Post a Comment