RC KUNENGE AKAGUA UJENZI WA KIWANDA CHA CHA KUZALISHA NYAYA ZA MKONGO WA MAWASILIANO HUKO MKURANGA

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe Abubakar Kunenge, amepongeza uwekezaji unaofanywa na kampuni ya Raddy Dibre Solution inayomilikiwa na wazawa katika kijiji cha Mwanambaya wilaya ya Mkuranga mkoani humo.

Pongezi hizo amezitoa Julai 28, 2021 wakati wa ziara ya kutembelea miradi inayowekezwa na wawekezaji kwenye wilaya ya Mkuranga ambapo alikuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza nyaya za mkongo wa wa mawasiliano (Optic Fibre Cable) kikiwa katika hatua za mwisho kabla ya kuanza uzalishaji.

Thamani ya uwekezaji wa kiwanda hicho kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha nyaya zenye urefu wa kilomita 24,000 kwa mwaka ni shilingi bilioni 17 na ujenzi wake utakapokamilika kitatoa ajira za moja kwa moja 400. 

"Napongeza uwekezaji huu, na ni vema viwanda hizi vifahamike, ni kiwanda muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu, hongereni sana kwa uwekezaji huu.".

Akieleza Changamoto inayowakabili  Mhandisi wa ujenzi wa kiwanda hicho Paschal Kasheku ameeleza kuwa wanasubiri kuunganishiwa gesi kutoka Shirika la Prtroli nchini (TPDC) ili waanze uzalishaji.










Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"