TORONTO, CANADA
MAAFISA nchini
Canada wamesema joto kali linaloikabili nchi hiyo kwa siku tatu mfululizo limesababisha
vifo vya zaidi ya watu 486.
Waziri Mkuu wan
chi hiyo Justin Trudeau ametuma salamu za rambirambi kufuatia vifo hiyo.
Katika mji wa
Britisha Columbia watu kadhaa wameripotiwa kufa na shughuli za dharura
zimedhoofu kutokana na ongezeko la watu waliokumbwa na janga hilo kali
lililokumba maeneo ya Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo na Marekani.
Tayari maeneo
ya ndani ya jimbo hilo watu wametaarifiwa kuondoka kufikia leo Jumsatano Julai
1, 2021 .
Mamia ya watu
wamefurika kwenye vituo 25 vya kupoza hewa jijini Vancouver ambapo watu
wameketi wakisoma vitabu na wengine wakiwa kwenye laptopa wakifanya shughuli
zao.
"Tumewahi kuwa na joto lakini sio la kiwango hiki cha
sasa," alisema Lou, ambaye alijitambulisha kwa jina moja tu. "Nimeshtushwa
kutokana na idadi kubwa ya vifo vilivyotokea."
“Sina kipoza hewa, ni feni tu, nimekuja hapa ili kupata
ubaridi wakati nafanya kazi zangu.” Alisema. Maeneo ya Magharibi mwa Canada
ndiyo yameathirika sana ambapo joto limefikia Nyuzi Joto 49.6. Mamlaka ya Hali
ya hewa nchini humo imeonya kuwa joto zaidi linakuja na kuwaasa wananchi
kuchukua tahadhari.
0 comments:
Post a Comment